Saturday, April 28, 2012

KABURI LA KANUMBA LAKARABATIWA



kabuli la kanumba lililoibwa mashada

‘ICON’ katika tasnia ya filamu Bongo, Irene Uwoya na mwenzake Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ hivi karibuni walimtafuta fundi na kwenda kulifanyia ukarabati kaburi la staa mwenzao marehemu Steven Kanumba.

Akizungumza na Ijumaa mmoja wa watu wanaojihusisha na kazi ya uchimbaji makaburi eneo la Kinondoni Dar, aliyejitambulisha kwa jina la Kidevu, alisema Ijumaa ya wiki iyopita alishuhudia mafundi wakilikarabati kaburi hilo huku Uwoya na Steve wakiwa pembeni.

“Baada ya lile kaburi kupasuka na kuanza kutitia, juzi niliwaona mafundi wakilikarabati huku pembeni wakiwa wamesimama waigizaji wawili yule mfupi anayeiga sauti ya Nyerere na Uwoya,” alisema Kidevu.
Akizungumzia hilo, Steve Nyerere alisema:
“Ni kweli mimi na Irene tuliamua kulikarabati kaburi la Kanumba baada ya kusoma gazetini kwamba limeanza kutitia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...