Tuesday, April 17, 2012

LULU KATIKA MAPAMBANO YA KUJIONDOA KWENYE MIKONO YA SHERIA.





  • APINGA UMRI ULIOTAJWA NA MWENDESHA MASHITAKA MKUU WA SERIKALI.
  • MAHAKAMA YAKELWA NA LULU KWA KUTOFUATA UTARATIBU.
  • WANASHERIA WASEMA HANA KESI YA KUJIBU.
MSANII wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ tarehe 11/04/2012 kwenye majira ya saa tano asubuhi alianza safari ndefu katika maisha yake ya mapambano, safari hii akijaribu kujinasua kwenye mikono ya sheria huku ajenda kuu ikiwa kuuonyesha ulimwengu tuhuma zinazo mkabili za mauaji ya msanii mwenzake si za kweli.
Lulu aliletwa mahakamani kwa siri huku akiwa chini ya uangalizi wa askari kanzu sita kati yao wawili wakiwa wanawake wakiwa na lengo la kumficha kwa watu pamoja na waandishi wa habari waliokuwepo mahakamani hapo wakimsubiri baada ya taharifa kupatikana kwamba angepandishwa kizimbani.
Akisimamishwa kizimbani mbele ya Hakimu Agustino Mmbando katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali, Beatrice Kaganda alidai kuwa Lulu ambaye ni mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam ana umri wa miaka 18.
Hatua ambayo Lulu aliipinga vikali na kuiambia mahakama kuwa ana miaka 17. Hapo ndipo aliposaidiwa kueleweshwa kuwa kwa utaratibu wa kimahakama apaswi kujibu lolote katika hatua za awali na vilevile Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji, lakini yeye aliona ni bora aanze kuweka utetezi wake vyema hata katika hatua hiyo ya awali
Kaganda aliendelea kumsomea mashitaka yanayomkabili ambapo alidai Aprili 7, mwaka huu eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam, alimuua mtu aliyejulikana kwa jina la Steven Kanumba. Kesi hiyo ilihailishwa na kupangiwa kutajwa tena Aprili 23, mwaka huu mahakamani hapo.
Askari kanzu wakisaidiwa na askari wa kawaida walimtoa Lulu mahakamani kupitia mlango wa nyuma moja kwa moja kwenye gari aina ya Suzuki Grand Vitara nyeupe yenye namba ya usajiri T848BNV, kwenye vioo vyake vya giza ilisomeka PT 2565 ambayo iliondolewa kwa haraka na kusadikiwa kumpeleka katika Gereza la Segerea.
MWELEKEO WA KESI.
Karata ya umri hiliyo chezwa na Lulu tayari inatoa mwelekeo wa kesi yenyewe na hivyo kumuweka marehemu -Steven Kanumba- ambaye alikuwa na umri wa miaka 28 katika hatia kulingana na sheria ya makosa ya kijinai yanayousiana na kujamiana. Hali hii inapunguza makali ya kesi ya mauaji na inaweza kumfanya asiwe na kesi ya kujibu.
Kwa umri wa miaka 17 ni mtoto na wala siyo mtu mzima hivyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye hata kama alipenda iwe hivyo unamfanya marehemu kuwa alikuwa anakusudio au alikuwa akimbaka na hivyo kuweka kesi ya mauaji kuwa na utetezi wa “self-defence” kwa maneno mepesi yanampa Lulu nafasi ya kumruhusu kujitetea kuwa alifanya lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake kujitetea dhidi ya mwanaumme mtu mzima aliyekuwa anamkamia kumbaka.
Inaelekea Lulu alishauliwa vema na swala la kubwatuka kwa umri alikuwa la bahati mbaya bali lilikuwa na lengo la kumpa haki yake ya kimsingi ya kuondolewa kwenye Gereza la watu wazima jambo ambalo mpaka sasa polisi wetu wameendelea kulikiuka.
Faida nyingine ya utetezi huu wa awali ni kufuta statement ambayo halihitoa mapema kwa madai ya kuwa polisi walimlazimisha kumshikilia kwenye korokoroni ‘Selo’ ya watu wazima na hivyo kumfanya aghafilike kiakili na kushindwa kutoa ushahidi sahihi, kwakuzingatia hilo ataiomba mahakama atoe ushahidi upya.
HOJA ANAZOWEZA KUJENGA KWENYE USHAHIDI MPYA
Katika ushahidi mpya Lulu ataelezea kuwa Marehemu ndiye aliyemwita na kudai kuwa ana mazungumzo nayeye ambayo ni muhimu yasiyo weza kungojea kesho yausuyo tasnia ya filamu. Hivyo yeye Lulu hakuwa na kusudio la kwenda kwa Kanumba kwa minajili ya kumwuuwa.
Ikumbukwe Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali ni lazima athibitishe nia ya kuua ili mahakama imtie hatiani Lulu lakini kama ni Kanumba ndiye aliyemwita mtuhumiwa nia ya Lulu kwenda kwa marehemu kwa nia tajwa itaota mbawa.
Lulu atathibitishia mahakama ya kuwa Kanumba akuwa mpenzi wake na kwa hivyo hoja ya Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali kuwa kulikuwa na ugomvi wa mapenzi kukosa mwelekeo.
Lulu atadai kilichomwangusha Kanumba chini na kukosa fahamu hakina uhusiano na yeye bali ni matatizo yake ya kiafya na atatumia taarifa ya madaktari wa Muhimbili kuthibitisha ya kuwa kilichomtoa roho marehemu ni mshtuko mkubwa katika ubongo wake (Brain concussion) ambao haukusababishwa na majeraha ya mwilini mwake ambayo hata hivyo hayapo. Marehemu hakuwa na jeraha lolote kuonyesha lingeweza kumsababishia mshtuko tajwa.
Lulu atadai mahakamani ya kuwa hakuna ushahidi wowote ule wa kitaalamu ya kuwa marehemu alikufa kwa lolote jinginelo tofauti na (Brain concussion) na inashangaza hata Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali kumfungulia kesi ya mauaji na hivyo kumbughudhi na kumdhalilisha mbele ya jamii na hivyo kuiomba mahakama iangalie namna ya kumfidia dhidi ya kubambikiziwa kesi ambayo hata haipo au “malicious prosecution”.
Lulu atashanga kwanini kwenye maelezo na vielelezo vya Mwendesha Mashitaka, Mkuu wa Serikali havikuonyesha afya ya marehemu ilikuwaje kwa sababu ajuavyo yeye alikuwa akitumia madawa mengi sana kila siku madawa yanayosadikiwa kuwa ni ya kupunguza makali ya vvu yaani ARV na huku akiwa na tabia ya kunywa pombe kali kama Jack Daniel, Konyagi, Whisky, Ram n.k.
Lulu atadai ya kuwa matumizi ya madawa tajwa na vinywaji vikali kwa wakati mmoja yalichangia katika kusitisha maisha ya marehemu na wala siyo yeye. Pia ataikumbusha mahakama kuwa anashindwa kuelewa ni vipi daktari wa marehemu ajashitakiwa kwa mauaji kwa kumpa marehemu madawa tajwa bila ya vibali vya hospitali zenye mamlaka ya kufanya hivyo…………
Lakini kubwa zaidi ni utetezi wa kimazingira ambao Lulu atautoa mahakamani utakao onyesha kuwa yeye ni mtoto wa chini ya miaka 18 na hivyo utamweka marehemu katika mazingira ya kiubakaji au kukusudia kumbaka na hivyo utetezi wa self-defence kuwa na uzito wa kipekee.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...