Wednesday, April 4, 2012

DIAMOND: WEMA AMEYATAKA MWENYEWE...





Baada kumdhalilisha Wema Isaac Sepetu mwishoni mwa wiki iliyopita, ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ (pichani) amesema kuwa mpenzi wake huyo wa zamani alijitakia mwenyewe. 
Akizungumza katika mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa, Wema alishindwa kusoma alama za nyakati kwani hakupaswa kunyanyuka kwenda kumtunza lakini kwa kuwa hakulifahamu hilo, ndiyo maana yakamkuta yaliyomkuta.
“Siwezi kumuomba radhi Wema,” alisema Diamond na alipoulizwa kwa nini asifanye hivyo akajibu:
“Aliyataka mwenyewe, siku hiyo mchana kuna vitu vilitokea na kabla sijaenda ukumbini so kama Wema angevikumbuka asingethubutu kufanya vile.”


MTITI ULIANZIA MBALI
Diamond anayewania Tuzo za Kili 2012 akiwa kwenye ‘kategori’ sita, alisema kuwa ishu haikuanzia pale ukumbini kwani Wema alimfuata mazoezini mchana wa siku hiyo, lakini hakuonana naye.
Alisema: “Nilipoamka asubuhi nilijiandaa na kwenda mazoezini, ghafla nilipigiwa simu na mtu nikaenda mahali, kabla sijafika huko nilipigiwa simu kuwa Wema amenifuata mazoezini, nilishangaa hivi huyu mwanamke vipi?

“Nikamwambia aliyenipigia simu kuwa sirudi hadi aondoke na kweli sikurudi hadi Wema alipoondoka.”

KUMBE NDIYE ALIYEMCHELEWESHA KWENYE SHOO
Diamond aliendelea kutambaa na mistari kuwa baada ya jaribio lake la kumfuata ukumbini kushindikana, Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, alitinga nyumbani kwake usiku akiwa ameongozana na rafiki yake wa kiume aliyemtaja kwa jina la Rommy.
“Nilimpigia simu Rommy aje nyumbani kuchukua tiketi ya kuingia kwenye shoo, nilishangaa aliponiambia kuwa Wema alimng’ng’ania na kuja naye nyumbani kwangu eti kuniomba msamaha, kiukweli alinivuruga hadi nikachelewa kwenye shoo.

DIAMOND ATAKA KUMSHUSHIA KIPIGO
“Nilikurupuka kwa hasira kwenda sebuleni kutaka kumpiga, namshukuru Mungu, mama na mjomba wangu walinizuia, mwisho wake mjomba akaamua kwenda kumwambia Wema aondoke,” alisema staa huyo wa kibao cha Moyo Wangu.

WEMA AJIBU MAPIGO
Baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha Diamond, Wema ambaye naye alijibu mapigo na kusema Diamond ni mswahili.
“Sikutegemea kama Diamond angekuwa mswahili kiasi kile, hadi kushindwa kuchukua fedha ambazo nilikuwa namtunza.
 “Nilikwenda ukumbini baada ya meneja wangu, Martin Kadinda kuniomba nikamuache pale.
Pia nilikwenda nyumbani kwa akina Diamond baada ya Rommy kuniomba nimpeleke akachukue tiketi yake.
“Nilipofika nyumbani kwao nilimuona mama yake Diamond akiwa nje, nikaenda kumsalimia, ghafla Rommy aliyekuwa ameingia ndani alitoka tukaondoka.”

WEMA ANUNUA MEZA KWA AJILI YA MASTAA  WENZIE
Katika kuonyesha kuwa fedha si kitu kwake siku ya shoo, Wema alinunua meza kwa ajili ya kukaa na mastaa wenzake.
“Siku ile nilikwenda kwa ajili ya kubadilishana mawazo na marafiki zangu ndiyo maana nikanunua meza kwa ajili ya kukaa na mastaa wenzangu kama Ray (Vincent Kigosi), Wolper (Jacqueline) JB (Jacob Steven) na wengine lakini kwa bahati mbaya hawakutokea,” alisema Wema na kuongeza:
“Kilichotokea pale ukumbini ni kwamba nilikwenda kutunza kama nilivyowatunza wengine.  Labda kujichetua kwangu ndiko kulikoniponza, unajua kuachana na mtu si kuwekeana bifu, ni jambo la kawaida.”

TUJIKUMBUSHE
Mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, Dar, kulifanyika shoo kubwa ya Diamond iliyokwenda kwa jina la Diamonds Are Forever ambapo Wema alikwenda kumtunza msanii huyo lakini jamaa akakataa kupokea fedha ya mrembo huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...