Monday, April 9, 2012

KANUMBA AMEACHA GUMZO KWA WAPENZI WA FILAMU TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA.



 Ni alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kipenzi chao kwenye tasnia ya filamu hapa bongo Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatcan. Chazo kinasema Kanumba alitoka kuoga na kumkuta Lulu ambaye inasemekana ni wapenzi akiongea na simu ndipo hapo ugomvi ulipoanzia mpaka kanumba kujikuta akidondokea kisogo na kutokwa na damu nyingi. Kwa sasa msanii wa kike Lulu anashikiliwa na police kwa maelezo zaidi

Watu wakiwa hawaamini kilichotokea 

 Hata mimi ilikuwa ngumu kuamini kwasababu nilikuwa nachat nae kwenye BBM hadi usiku na kumuuliza sikukuu hii bata tunalila wapi, halafu msg ya mwisho aliniambia kuwa anataka na mimi siku moja niingie kwenye filamu yake daaah.

Msanii Shilole akiwa hajielewi kabisa akiingia nyumbani kwa Marehemu 

Rafiki mkubwa wa marehemu anaitwa Tito yeye ndio alikuwa na mwili wa marehemu hadi hosp ya Mwimbili  

Msanii Johari akiwa kwenye huzuni kabisa akifanya mahojiano ya TV  

 Kijana huyu yeye alipopata habari pale pale alianguka chini

H.Baba akiwasili nyumbani kwa Marehe Steven Kanumba 

Steve Nyerere akiwasili nyumbani kwa marehemu akiwa kwenye majonzi mengi 

Swahiba mkubwa wa Kanumba Ray akiwa mwenye huzuni nyingi 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...