Saturday, April 14, 2012

ETI “WEMA SEPETU” ALITAKA KURUDIANA NA MAREHEMU KANUMBA…!!






BAADA ya kutokea kwa kifo cha kinara wa filamu Tanzania Steven Kanumba, malkia wa skendo Wema Sepetu, amekaliliwa akisema kuwa tayari walikuwa na mpango wa kurudiana kimapenzi na Kanumba kwani siku mbili nyuma kabla ya kifo chake walikuwa tayari wameanza kuwasiliana.

Wema alitoa kauli hiyo pindi alipokuwa akizungumza na waandishi mbalimbali wa habari nyumbani kwa marehemu Vatican Sinza.

“Yani Kanumba ni mtu ambaye alinitoa katika tasnia hii ya filamu, na tayari tulikuwa tumeanza kuzungumza juu ya kurudiana katika mahusino yetu yani sijui niseme nini naumia jamani,” alisema huku akitokwa na machozi pamoja na kwikwi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...