Wednesday, April 4, 2012

Mastaa wafanya kufuru...






KITCHEN Party ya msanii wa filamu Bongo, Jaji Khamis ‘Kash’ ni kufuru tupu kuanzia vyakula, vinywaji, mavazi na wasanii kushindana wenyewe kwa wenyewe...

Sherehe hiyo ilifanyika Ijumaa Machi 30, mwaka huu, katika Ukumbi wa Vijana, Kinondoni Dar es Salaam na kufunikwa na vituko vya kila aina vya wasanii...
HUKU KASH KULE MAYA
Majira ya saa mbili usiku, Kash aliingia ukumbini humo akiwa na mpambe wake, Mayasa Mrisho ‘Maya’ aliye memba wa filamu Bongo na kushangiliwa na wageni waalikwa huku shughuli nzima ikitiwa nakshi na Mc Jojoo.
VYAKULA, VINYWAJI
Ukiachana na namna ya upambaji mzuri wa ukumbi huo, vyakula na vinywaji vilikuwa vya kumwaga na waalikwa walikula hadi kusaza na kuogelea vinywaji.

WASHINDANA MAVAZI
Upande wa mavazi ilikuwa ni mashindano ya hali ya juu, lakini wasanii wa Klabu ya Bongo Movie walionekana kufunika zaidi.

Wasanii hao walikuwa wamevaa sare ya kitenge lakini kila mmoja alishona kwa staili yake ingawa wengi walivalia viguo vifupi vyenye kuacha sehemu kubwa ya miili yao nje.

Jacqueline Wolper ndiye aliyefunika zaidi kwa kushona kitenge hicho kwa mtindo wa kaptura fupi na blauzi yake.

WASHINDANA KUCHEZA
Kinywaji kilipowafikia mahali pake, wasanii wa Bongo Movie walianza kushindana kucheza muziki kwa mtindo wa kuweka duara halafu mmoja kuingia kati na kuyarudi.

Katika mchuano huo usio rasmi, Wolper alionekana kufunika zaidi ingawa alikuwa akipepesuka kutokana na kulemewa na kilevi kichwani, akifuatiwa kwa mbali na Jenifer Kyaka ‘Odama’.
WOLPER AWA PEDESHEE
Wakati wa zoezi la utoaji zawadi, Wolper ndiye aliyefunika zaidi kwa kumwaga noti za ‘msimbazi’ nyingi na kushangiliwa na wasanii wenzake.
K
ASH ALONGA
Shughuli ikikaribia ukingoni, Kash alisimama na kuwashukuru wasanii wenzake wote waliomuunga mkono pamoja na wageni waalikwa.

“Huu ndiyo umoja wa kweli, sina cha kuwalipa marafiki zangu, lakini nasema ahsanteni sana kwa moyo mliouonesha kwangu, tuzidi kushirikiana.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...