Tuesday, April 17, 2012

MAMA, BINTI ZAKE WAVUA NGUO HADHARANI


Sara Butler akiwa na wanae wakisali.

Sara na wanae wakitolewa eneo la tukio na Wanausalama.

MAMA mmoja aliyefahamika kwa jina la Sara Butler (43) mkazi wa kitongoji cha Upper Darby jimbo la Philadelphia nchini Marekani yeye na wanaye wanashikiliwa na Polisi wa nchini humo baada ya kukutwa wakisali mbele ya shule wakiwa uchi wa mnyama.

Taarifa kutoka polisi zinasema kuwa Sara Butler akiwa na wanae wa kike Joann (23) na Bessie 22 pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14 walisaula nguo zao zote na kubaki kama walivyozaliwa kisha wakaanza kusali kwenye maegesho ya magari mbele ya shule.

Taarifa zaidi zilisema kuwa awali siku ya tukio, mama huyo na wanaye walifika kwenye Shule ya Sekondari ya Upper Darby, ambapo walienda kumuona mwanafunzi mmoja aliyedaiwa kuwa ni mmoja wa familia yao.

Ilidaiwa kuwa walipofika shuleni hapo walikataliwa kukutana na mtoto huyo kwa sababu haikuwa sheria ya shule.

Sara alipoona amekataliwa kumuona mwanaye huyo aliamua kuwakusanya watoto wake ambapo aliondoka na kwenda kwenye maegesho ya magari ya shule na kuanza kufanya ibada huku wakiwa wamevua nguo.

Hali hiyo iliwashangaza watu wengi kwani walihisi mama na watoto wake wanaweza kuwa na upungufu wa akili.

Sakata halikuishia hapo mama huyo aliamua kupanda juu ya gari ili aonekane vizuri, lakini kabla hawajamaliza sala yao waliyokuwa wameikusudia polisi walitinga eneo hilo baada ya kutonywa.
Mama huyo na wanae wanaozidi umri wa miaka 18 walifunguliwa mashtaka ya kuvunja maadili ya jamii na kujianika uchi hadharani.

Hata hivyo, Sara na wanaye walipelekwa kwa daktari wa wagonjwa wa akili ili kupimwa kama kichwani zimo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...