Friday, April 27, 2012

Wema, Kajala wapatana gerezani...



STAA kwenye sinema za Bongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni alivunja ukimnya kwa kuamua kutinga Gereza la seregea, jijini Dar es Salaam kwa madhumuni ya kumuona mahabusu Kajala Masanja na kuondoa tofauti zao Amani lina ishu nzima.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Wema alitinga gerezani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa ameongozana na Mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds Tv, Zamaradi Mketema.

Mikononi mwa wawili hao kulikuwa na ‘mapochopocho’ mbalimbali kama zawadi kwa mahabusu huyo.
“Kwa kweli hatukuamini kumwona Wema akiingia gerezani kwa lengo la kumuona Kajala kutokana na vita yao siku za nyuma, tulijua alikwenda kwa Lulu, ila tulipoambiwa yuko na Kajala tena wote wanalia ndiyo tukaamini,” alidai shuhuda huyo.

Alisema kuwa kilio cha wawili hao kilitokana na kukumbushana habari za kifo cha Kanumba na jinsi walivyojengeana uadui hapo awali.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa kilio chao kilisitishwa na afande mmoja aliyemtaka Wema kutoka nje.
Baada ya kupata taarifa hizo, paparazi wetu alimpigia simu Wema na kumuuliza kuhusu madai ya kumaliza tofauti zao ambapo alijibu:

 “Yeah, ni kweli. Kuna sababu kuu mbili zilizosababisha kuangua kilio pale gerezani, kwanza kutoonana kwa muda mrefu na Kajala.

“Pili kuna maneno aliniambia ya Kimungu na kunisihi jinsi ya kuishi na watu, tukamkumbuka na Kanumba,” alisema Wema.

Wawili hao walikuwa marafiki wakubwa, lakini pepo wa matengano akaingia katikati yao na kuwa maadui.

Kajala alipotupwa gerezani, wasanii mbalimbali walijitolea kutoa michango kwa lengo la kumsaidia mtuhumiwa huyo kisheria, lakini familia ya Kajala ilidaiwa kuukataa mchango wa Wema kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mnafiki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...