Friday, April 20, 2012

HIKI NDIO ALICHOSEMA MWIGIZAJI RAY KUHUSU KUHUSISHWA NA KIFO CHA KANUMBA.



.
Baada ya stori kuenea kwamba Mwigizaji RAY anahusika moja kwa moja na kifo cha mwigizaji STEVEN KANUMBA, mwigizaji huyo amezungumza exclusive kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM.
Amesema “nimekua nikizisikia sana hizi tuhuma, sio kweli kwa sababu Kanumba ni mdogo wangu wa karibu sana tumetoka mbali sana kimaisha mimi na yeye, nimekua na mazoea ya kuona vitu kila siku vinaandikwa ambapo juzi nilipigiwa simu na kuambiwa nitazame kwenye blog ya U Turn ambayo anaimiliki huyu dada ambae simfahamu anaitwa Mange Kimambi”
“Alikua ameandika kwamba amepata taarifa kutoka kwa polisi mmoja wa Osterbay kwamba Ray ndio aliepiga simu kwa Lulu siku ya kifo cha Kanumba kwa hiyo Lulu ametumika kufanya mauaji bila kujijua, na pia kukawa kuna swali kwamba kwa nini Ray alikua wa kwanza kufika kwa marehemu Kanumba, Mungu ndie anaejua” – Ray
Kwenye sentensi nyingine, Ray ameamplfy kwamba “kwa hiyo anataka kuwadhihirishia watanzania kwamba Ray ndio anahusika na hicho kifo, baada ya hilo nimeshirikiana na polisi na kushitaki na kufungua kesi ambapo hivi sasa ninapozungumza yupo polisi Osterbay akihojiwa kwa sababu ameandika kitu ambacho bado kipo ndani ya uchunguzi, hana uhakika nacho sijui Luli amekamatwa Coco Beach which is not true, sijui hizi habari kaipata wapi”
Akionyesha kuumizwa, Ray aliongeza kwamba “sasa hii ni kutaka kunivunjia heshima, mimi nafanya kazi ya kuigiza ndio maisha yangu unapoandika kitu kama hicho kwenye internet inafika sehumu kubwa dunia nzima, sasa unategemea watu wanichukuliaje kama sio kunivunjia heshima, kunipotezea mashabiki wangu… nasema hili sitoweza kuliacha, nitalifanyia kazi na nitalifikisha mahakamani ili iwe fundisho, sitolichekea”
Kwenye sentensi nyingine Ray ameamplfy baadhi ya maoni yaliyotolewa na watu mbalimbali kwenye hiyo habari iliyoandikwa kwenye hiyo blog, amesema “maoni niliyoyasoma mengine yanamwambia yule dada kwamba anachokiandika kinaweza kumcost kwenye maisha yake, na nyingine zinasema kwamba tuko tayari kumvamia Ray na kumuua, sasa hichi kitu ni hatari sana kwenye maisha yangu kwa hiyo nimemshitaki polisi na kuandika kwa kusema chochote kitakachonikuta hata nikipigwa jiwe na kuanguka mimi nadili na huyo mwanamke kwa sababu yeye ndio mtu aliepublish hivyo vitu watu wanichukulie mimi vinginevyo kabisa tofauti jinsi nilivyo na sihusiki kabisa na hicho kifo, kimsingi maisha yangu yapo hatarini lakini nasema haya ni maisha nitaendelea kuvumilia”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...