Friday, August 19, 2011

BALAA...!!!!!




MWANAMKE mmoja jijini Dar es Salaam ambaye hakufahamika jina lake, amekutwa na balaa ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kudaiwa kufanyiwa kitu mbaya na kutelekezwa barabarani.

Tukio hilo lilijiri jirani kabisa na Makao Makuu ya Runinga ya TBC1 Bamaga jijini Dar Jumatatu wiki hii saa 2: 00 asubuhi na kushuhudiwa na watu kibao waliokuwa wakiwahi ‘makazini'.

Muda mfupi baada ya tukio hilo, ‘vuvuzela’  alitimba mahali hapo na kumkuta mwanamke huyo aliyeonekana kuwa ni mke wa mtu akiwa hajitambui.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwanamke huyo alishushwa kwenye gari aina ya Toyota Coaster na kutelekezwa eneo hilo ambapo alikuwa akiyumba na baadaye alidondoka akionekana kulewa kupita maelezo.

“Alishushwa na mwanaume mmoja, ghafla nilishangaa kuona gari likiondoka kwa kasi ya ajabu,” alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Amri.





Shuhuda huyo aliongeza kwamba, kwa jinsi mwanamke huyo alivyoonekana, alikuwa ameleweshwa madawa ya kulevya au pombe hivyo ili kukwepa msala, mhusika alimtupa eneo hilo na kuingia mitini.

Hata hivyo, tulitaka kujua mkasa ulimpata mwanamke huyo, hakuweza kuzungumza chochote kwa namna alivyokuwa ‘amechoka’.





Pamoja na kufanya jitihada za kumwamsha, lakini hadi gazeti hili linaondoka eneo la tukio, mwanamke huyo alikuwa hajazinduka.

Vitendo vya watu kuleweshwa na kufanywa watumwa wa ngono au kuuawa vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara hivyo tunawashauri kuwa makini kila wanapokwenda.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...