Thursday, August 25, 2011

‘Twanga Pepeta’



Kikosi kamili cha Bendi ya African Star  International ‘Twanga  Pepeta’ leo  kinatarajiwa  kuteremsha  burudani nzito ya kukata na shoka  ndani ya Ukumbi  wa Mawenzi  Garden  Tabata  jijini  Dar.

Akizungumza na  gazeti hili juzi, mratibu wa  onesho hilo, Sauda Mwilima,  ‘Top Queen’ alisema shoo ya wakali hao iliyopewa  jina la  ‘Usiku wa kusugua  kisigino’ itakuwa  kali  kutokana na maandalizi  yaliyofanywa  hasa  ukizingatia  kuwa  litakuwa onesho la kwanza  kwa mwaka  huu  katika ukumbi huo.

“Hili ni onyesho la kwanza kwa wakazi wa Tabata katika mwaka huu wa 2011, kwa maana hiyo bendi imejipanga  kuhakikisha inafanya makubwa  na kuacha simulizi kwa wakazi wa maeneo hayo,”  alisema  Sauda na  kuongeza  kuwa  kiingilio katika  shoo hiyo iliyopangwa  kuanza saa tatu usiku  kitakuwa  ni ‘buku’ tano tu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...