Sunday, August 28, 2011

HATARI...




MAPENZI kutoka moyoni ni simulizi kwa mastaa wengi Bongo, nyanyuka nikae ndiyo zao kama kupishana siti za daladala, mtindo ni kujihudumia a.k.a self service.

Mtindo wa kuzungukana na kuchukuliana wapenzi na wachumba siyo stori kwao, warembo kadhaa wameshakutana kwa wanaume zaidi ya mmoja na kuchangia penzi, wakanuniana kwanza, baadaye urafiki wa mashaka ukaendelea.





AUNT NA WEMA
Staa wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ na Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu wanadaiwa kukutana kwenye penzi la mjasiriamali maarufu Bongo, Jack Pemba.

Pamoja na madai hayo, Wema amekuwa akikanusha kutoa penzi kwa Pemba ingawa vyanzo vya habari vinasisitiza.

Kwa sasa, Pemba ambaye aliigiza na Aunt katika filamu ya Miss Bongo, amejinasua kwenye mapenzi na warembo maarufu, hivi sasa ametulia na mwenzi wake ambaye hana jina kubwa mjini.

Aunt na Wema, pia walikutana kwenye penzi la Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Hartmann Mbilinyi ambaye kuna kipindi alinusurika kuugua uchizi kwa mapenzi ya warembo wauza ‘nyago’ kwenye filamu.

AUNT NA SARA
Aunt anaendelea kutengeneza ‘paragrafu’, kwani anatuhumiwa kuingia kwenye anga za muigizaji mwenzake, Sara Mwakapala ‘Bukabi’ na kumchukulia mchumba wake, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’.

Sara alidai kumfumania Aunt chumbani akiwa na Silva, baada ya hapo mrembo huyo alibaki na ujauzito ambao ameshajifungua, huku baba wa mtoto akiendelea kujidai na Gwantwa.





JACK PENTZEL NA WEMA
Staa mwenye ‘kashkashi’ za wanaume, Jacqueline Pentzel anadaiwa kukutana na Wema kwenye penzi la muigizaji maarufu Bongo, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’.
Kwa awamu hiyo, Wema anakanusha kutoka kimapenzi na Chuz, ingawa vyanzo vinasisitiza ukweli wa data zenyewe.

Jack na Wema ambao wanajidai ni marafiki wakubwa, wanadaiwa kukutana kwenye penzi la staa wa African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Mbwana ‘Charlz Baba’ ambaye ni mzazi mwenza wa mshindi namba mbili wa Kimwana Manywele 2007, Husna Idd ‘Sajent’.

Hata hivyo, kwa hapa Jack ndiye anakunusha, ingawa ameshindwa kujitoa kwenye skendo hiyo.





KIRUNGU CHA MR. CHUZ
Wema na Jack siyo peke yao ambao wamo kwenye orodha, wasanii wenye majina makubwa Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’, Joan Matovolwa na Leila Ismail ‘Lily’ kwa nyakati tofauti pia wamepitiwa na kirungu cha Mr. Chuz.

WEMA NA WOLPER
Hivi sasa Wema anaweka wazi kwamba amejituliza kwa mkali wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ lakini janki huyo huyo amesharipotiwa kuchakachua na nyota wa filamu, Jacqueline Wolper.

Mshiriki wa Miss Kiswahili, Rehema Fabian naye ameshajitangaza kuwahi kutoka kimapenzi na Diamond kama ilivyo kwa mshiriki wa Shindano la Maisha Plus Season II, Upendo Moshi.





MAINDA NA JOHARI
Mastaa wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’, wao siyo stori kwamba wamekuwa ‘wakinyang’anyia’ penzi la galacha wa sanaa za maigizo nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Kwa upande mwingine, Ray ameshahusishwa kutoka kimapenzi na mtangazaji maarufu Bongo, Joyce Kiria ingawa hakuna mmoja kati yao aliyewahi kujitokeza kupinga wala kukubali.

UWOYA NA JACK PATRICK
Staa wa filamu, Irene Uwoya Ndikumana ‘Mama Krish’ kabla hajafunga ndoa anadaiwa kuchangia penzi na Miss Ilala namba tatu 2005, Jacqueline Patrick ‘Jack wa Chuz’.

Mwanaume aliyedaiwa kuwagonganisha ni dalali wa magari, Ifraj Haroub ambaye ni mtoto wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Koani, Haroub Masoud.

Ifraj, alisharipotiwa kutoka kimapenzi na mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid, ikiwa ni pamoja na picha zao ‘wakichakachua’ dhambi ya zinaa kuanikwa.






UWOYA NA QUEEN SUZY
Skendo ilivuma kwamba Uwoya akiwa ndani ya ndoa, pia alitoka kimapenzi na nguzo ya Bendi ya Mapacha Watatu, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’.

Ishu hiyo, ilisababisha ugomvi kati ya staa huyo wa filamu na aliyekuwa mchumba wa Kalala, Mary Junior ambao ulitimka Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam.

Kashfa hiyo, inakwenda mbali zaidi na kuzalisha tawi kwamba Uwoya aliwahi kuchangia penzi na mnenguaji Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ anayedai amezaa na Kalala ambaye anamkana mtoto.

UWOYA NA FLORA
Uwoya amewahi kutoka kimapenzi na mwanamuziki Hamis Baba ‘H Baba’ ambaye kwa sasa amejituliza kwa msanii wa filamu, Flora Mvungi.

KAJALA NA RAY C
Muigizaji Kajala Masanja amewahi kuripotiwa kupigana na mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, wakigombea penzi la prodyuza maarufu wa Bongo Fleva, Paul Matthysse ‘P Funk’.

Kajala ni mzazi mwenzake P Funk, wakati Ray C baada ya hapo alijiweka kwa staa wa Big Brother, Mwisho Mwampamba kabla ya kutua kwa memba wa Kundi la Nako 2 Nako, Isaac Waziri Makuto lakini wote walishamwagana.





SYLVIA, LISA, NARGIS
Mamis Ilala, Nargis Mohamed (2003) na Sylvia Shally (2009), Miss Tanzania namba 3 2006, Lisa Jensen na muigizaji, Shamsa Ford wamewahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘taikuni’ wa Bongo Movie, Steven Kanumba. Hata hivyo, Lisa anakanusha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...