Thursday, August 25, 2011

MKE AMLIPUA MUMEWE SEHEMU ZA SIRI

Mwanamke mmoja mwenye wivu wa mapenzi, Victoria Bynes (29) (pichani), amejikuta matatani baada ya kufikishwa mahakamani baada ya kuzichoma moto sehemu za siri za mumewe kwa kushuku kuwa ana kimada.

Habari za awali zinasema mwanamke huyo alichukizwa baada ya mume wake, Andrew Williams kulala nje ya ndoa kwa siku saba bila kurudi  nyumbani na  aliporudi alichukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye chupa na kummwagia sehemu za siri kabla ya kutumia kibiriti kuwasha moto ulioteketeza sehemu nyeti za mwanaume huyo.



“Wakati mwanaume huyo akihangaika kuuzima moto uliokuwa ukiteketeza sehemu zake nyeti, Victoria alipanda gari lake na kuondoka bila kumpa msaada wowote,” kilieleza chanzo cha habari.

Habari zinasema polisi walipoitwa walimkuta Williams akiwa ameungua vibaya sehemu za siri pamoja na tumbo lake, sasa yuko hoi amelazwa hospitali.

Ilielezwa kuwa sababu za mwanamke huyo kumchoma moto Williams ni kushuku kuwa ana kimada kwa vile hakurudi nyumbani wala kuwasiliana naye kwa muda wa wiki moja.





Tayari Victoria amefikishwa mahakamani kwa kosa hilo na alipoambiwa na hakimu ajitete alisema kuwa anajuta kwani aliziwasha moto nyeti za Williams kwa bahati mbaya, lengo lake lilikuwa kumtishia kuzichoma.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...