Wednesday, August 24, 2011

Washiriki BSS waonesha utamu wa faragha




Mwapwani Yahya na Bella Kombo ambao ni washiriki wa shindano la kusaka vipaji vya muziki, Bongo Star Search (BSS) wametia doa baada ya kupanda jukwaani wakiwa na vivazi vinavyoonesha maungo yao.

Mwapwani (pichani juu) na Bella (pichani chini) walivaa nguo ambazo zilikuwa zinaonesha kila kitu ndani, ingawa kila mmoja aligonga ya mtindo wake.

Tukio hilo lilichukua nafasi Jumatano iliyopita kwenye Ufukwe wa Mbalamwezi, Dar ambako washiriki wa BSS walipanda jukwaani kukamua mbele ya majaji, huku wakirekodiwa kwa ajili ya kurushwa hewani na Runinga ya ITV, juzi.

Mwapwani yeye alivaa kinguo kilichoonesha mpaka juu kabisa ya mapaja, wakati Bella yeye mwili mzima ulikuwa ‘kideo’, kwani kwa kila aliyemsogelea aliona utamu wote wa faragha.

Katika shindano hilo ambalo mwaka huu linaitwa Second Chance kwa maana ya kuwapa nafasi ya kushindana mara ya pili wale waliojitahidi misimu iliyopita lakini wakakosa nafasi, Mwapwani ndiye aliyeaga huku akiwaacha Mary Banyuka na Imani Lisu katika kona ya hatari (danger zone).

 Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen ‘Madam’ ambaye ni mratibu wa shindano hilo, amepongezwa kwa kuifikisha BSS patamu ikiwemo hilo la kuwapa nafasi ya kushindana mara ya pili wote walioshindwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...