Saturday, August 6, 2011

MTOTO WA ASKOFU ATIKISA JIJI..


Huku kukiwa na fukuto juu ya madai ya utajiri wa kutisha wa baadhi ya viongozi wa dini, mtoto wa Askofu wa ‘Ministri’ ya Ngurumo ya Upako, Nabii Geordavie, Nick Davies anayejiita ‘Usher Raymond wa Bongo au Nicksher’, anadaiwa kulitikisa Jiji la Arusha kwa matanuzi.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha gazeti hili, Nick ambaye ni muimba injili anayetumika katika kanisa linalosimamiwa na baba yake, amekuwa ‘akisengenywa’ na baadhi ya wakazi Arusha eti, anabadilisha magari na pamba za kisharobaro balaa hivyo kutengeneza picha f’lani katika jamii.

Ilidaiwa kwamba, awali mtoto huyo wa Nabiii ambaye pia ni prodyuza wa nyimbo za Injili, alikuwa na gari aina ya Toyota Mark II, lakini kwa sasa anasukuma  mkoko mwingine wa maana aina ya Toyota Celica.
NICK ANASEMAJE?


“Hujakosea, kweli naitwa Nick, ni mtoto wa Nabii Geordavie wa Ngurumo ya Upako Arusha. Pia ni kweli natumia jina la Usher Raymond wa Bongo. Nimekusiliza vizuri, lakini nashindwa kuelewa hizo tetesi ni nani aliyezileta kwenu mana’ke nikiangalia madai ya kwamba natanua sana au nalitikisa jiji kama ulivyoniambia, mimi nafikiri hayo ni maneno tu.

“Ukweli ni kwamba nina studio yangu hapa Arusha, huwa nafanya kazi ya kurekodi nyimbo za wasanii mbalimbali. Pia ni mpiga vyombo mzuri, sasa tukiongelea matumizi ya fedha, nadhani utaelewa kabisa kwamba zinatokana na miradi yangu na baba hausiki hata kidogo.



“Pamoja na kwamba baadhi ya watu watakuwa hawaelewi, ila naomba wafahamu kuwa, tofauti na kazi ya studio, huwa natengeneza ‘jingo’ za matangazo ya kampuni mbalimbali hivyo kujiingizia kipato.
“Kuhusu suala la kuendesha magari, lipo nje ya uwezo wangu kwa sababu gari nililonalo nilipewa na wazazi wangu na ndiyo wanaoweza kulizungumzia hilo.”

WAUMINI WAFUNGUKA MADAI YA UTAJIRI WA VIONGOZI WA DINI
SUZANE KIBENA

Muamini huyo wa Kanisa la Full Gospel chini ya Askofu Zachary Kakobe alisema: “Si vema kuwasema watumishi wa Mungu kwani wanatuunganisha na Mungu.”


DAUD KIWELA
Muumini huyo wa Kanisa la Assembles Of God chini ya Mchungaji Getrude Rwakatare alikuwa na haya: “Sifahamu utajiri wa mama kwa hiyo sijui kama unatisha au la.”
KAKUU MELAU
Kutoka katika Kanisa la Living Water ‘Makuti Kawe’ chini ya Nabii Onesmo Ndegi, muumini huyo alisema: “Zamani ilikuwa ukiwasema vibaya watumishi wa Mungu, unapigwa ukoma lakini kama kweli wapo wanaojilimbikizia mali, waache.”

EBENEZER URASSA
Muumini huyo wa Kanisa la Maombezi chini ya Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ alisema: “Wajaribu kuishi maisha sawa na waumini wao ili kuondoa tofauti.”
SALOME PETRO ‘DUZA’
Kwa upande wake muumini huyo wa Kanisa la Huduma ya Hakuna Lisilowezekana chini ya Askofu Sylvester Gamanywa alisema: “Afanyaye madhabahuni hula madhabahuni, lakini hao ambao wamepitiliza wanapaswa kujiangalia upya.” 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...