Tuesday, August 16, 2011

WAPIGIE KURA WASANII WA BONGO FLEVA TUZO ZA MUSEKE ONLINE AFRICA AWARDS (MOAMA)




CPWAA, mmoja wa wafalme wa muziki wa Bongo Fleva (Bongo Crunk), ni miongoni mwa wanamuziki wa bongo fleva wanaowa tuzo za muziki Afrika za Museke Online Africa Awards (MOAMA) kutoka katika kundi la “Chaguo la Wapiga Kura” ambalo linajumuisha wasanii kutoka nchi 58 za Afrika kwa kupitia Akademia ya ma-DJ, mitandao mbalimbali na tasnia za burudani.  Uchaguzi huo hufanywa kwa kuwachagua wasanii bora katika kila nchi kupitia mtandao.
 Wasanii wengine wa Tanzania waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Shaa, Temba, Chege, Diamond, ambapo Hermy B amechaguliwa kama prodyuza bora zaidi kwa upande wa kurekodi kanda za sauti na Adam Juma amechaguliwa kwa kuwa mkurugenzi bora zaidi wa video.
 Utoaji wa tuzo hizo utafanyika jijini New York, Septemba 24, mwaka huu na kutangazwa moja kwa moja na tovuti ya Museke na channel za muziki za Afrotainment. Ili kumpigia kura C-pwaa na wengine, fungua mtandao wa :www.moamas.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...