Saturday, August 13, 2011

MASIKINI VENGU


MASIKINI Vengu! Ndiyo neno linaloweza kukutoka mara utakapopata taarifa za hali ya afya ya mchekeshaji huyo maarufu Bongo, anayepiga mzigo ndani ya Kundi la Orijino Komedi, ambaye jina lake halisi ni Joseph Shamba.

Staa huyo mwishoni mwa wiki iliyopita alikimbizwa katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni, Dar akiwa hajitambui kutokana na hali yake kiafya kuwa mbaya.

Habari kutoka chanzo chetu zinatonya kwamba, Vengu alifikishwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa ghafla ambapo baada ya vipimo vya madaktari ilithibitika kwamba anasumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

“Yupo Kairuki (hospitalini), hali yake si nzuri kabisa, alifika hospitalini akiwa haongei, haoni wala hajitambui,” kilieleza chanzo hicho kikiomba kuhifadhiwa jina lake.

Paparazi wa BLOG hili alifunga safari hadi ilipo Hospitali ya Kairuki na kuthibitisha kuwa ni kweli alikuwa amelazwa hospitalini hapo ingawa hakupata nafasi ya kumuona.
Kikubwa ni kumuombea staa huyu ili apone haraka.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...