Tuesday, August 2, 2011

LULU APEWA KIBANO...



Binti anayefanya vizuri kupitia tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepewa kibano na mama yake akitakiwa kupunguza kujirusha na kurudi kuishi nyumbani kwao Tabata kama ilivyokuwa huko nyuma.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na madai kuwa, msanii huyo amekuwa na tabia ya kulala kwa marafiki zake ovyo kila anapotoka usiku kwenda kujirusha.



Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, kufuatia agizo hilo sasa hivi Lulu anaishi Tabata na amekuwa hayuko huru kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

“Mama yake kampa kibano, hataki aende kujirusha na kulala kwa marafiki zake ovyo, mwenyewe anaichukia sana hali hiyo kwani amezoea kuwa huru zaidi,” alidai mtoa habari huyo.

Lulu ambapo alipopatikana alifunguka: “Ni kweli naishi na mama yangu sasa hivi na kiukweli naenda klabu mara moja moja sana, ni maisha tu.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...