Friday, August 5, 2011

BOB JUNIOR: MIMI SIYO SHOGA, NI USANII...



Prodyuza ambaye pia ni msanii anayefanya vizuri kunako gemu la muziki wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ (pichani) amefunguka kuwa, yeye si shoga ila kazi yake ndiyo inamfanya awe kama alivyo.Bob Junior alisema kuwa, baadhi ya watu wamekuwa wakimtafsiri tofauti kutokana na muonekano wake bila kujua kuwa, usanii ndiyo chanzo.

Alisema kuwa, yeye ni mwanaume kamili na watu wasiende mbali katika kujadili muonekano wake na kumuingiza kwenye ushoga bali watathmini burudani anayotoa.

“Watu wanashindwa kuelewa kama usanii ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, lazima mtu uwe tofauti kuanzia muonekano, mavazi na hata staili yako ya kutoa burudani kwa mashabiki, kama ni shoga mbona hata leo tu nilikuwa na baby wangu?” alisema Bob Junior.

Hivi karibuni ililiripoti kuwa, Bob Junior alibambwa maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian lakini wawili hao walipohojiwa hawakuweka wazi uhusiano wao licha ya huko nyuma kudaiwa kutoka kimapenzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...