Saturday, August 20, 2011

FUMANIZI: BABA, BINTIYE LAIVU...

Ama kweli dunia imekwisha! Baba mmoja ambaye ni meneja wa baa maarufu iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Richard, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya mwaka baada ya
kufumaniwa akiwa na binti yake wa kumzaa... Tukio hilo la kufedhehesha lililoshuhudiwa na umati lilitokea mchana wa Agosti 17, mwaka huu maeneo Ubungo Kibo jijini Dar es Salaam.

MCHEZO ULIVYOANZA
Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio kilidai kuwa, awali baba huyo mwenye mke na watoto alikuwa akimmendea binti yake mwenye umri usiozidi miaka 15 (jina tunalihifadhi) akimtaka kimapenzi.

“Yule mtoto alikuwa analalamika kuwa baba yake anamtaka, alichokifanya alimwambia mama yake ili amsaidie jinsi ya kukabiliana na vishawishi hivyo,” kilidai chanzo hicho na kuongeza.




“Mama yake hakuamini yale aliyoambiwa, maelezo yale yalimchanganya sana lakini baadaye akaamua kuwashirikisha ndugu na majirani.”

TAARIFA ZINAPELEKWA KWA MJUMBE
Ilielezwa kuwa, baada ya mama mzazi wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina moja la Shoro kuwapasha majirani zake juu ya tabia hiyo ya mumewe, walimshauri aende kutoa taarifa kwa mjumbe wa shina, mzee Omari (aliyenyoosha kidole pichani).





“Taarifa zilipofika kwa kiongozi huyo, kwanza alishangaa lakini baadaye yeye kwa kushirikiana na ndugu pamoja na majirani waliamua kuzithibitisha tuhuma hizo kwa kuandaa fumanizi,” kilinyetisha chanzo hicho.

MTEGO WAWEKWA
Inadaiwa kuwa, katika kufanikisha zoezi hilo, binti huyo ‘alisetiwa’ ili atakapotakiwa kimapenzi na baba yake amkubalie lakini kabla ya mchezo, awashtue kimtindo.







“Mtoto alipewa mbinu za kufanikisha fumanizi hilo, siku ya tukio mama akaaga anakwenda kliniki, akamuacha mtoto na baba yake ndani, huko nyuma yule baba akaanza kuomba ‘mambo’.

“Kama alivyoelekezwa, binti akakubali, wote wakavua nguo lakini baada ya muda aliwashtua kwa simu watu waliokuwa wamebana sehemu ambao muda mfupi walivamia chumba hicho.

BABA, BINTIYE LAIVU
Ilielezwa kuwa, baada ya watu kuvamia akiwemo mjumbe, wawili hao walikutwa wakiwa watupu hivyo kuzua timbwili zito.
“Palichimbika! Mjumbe akaanza kumchapa bakora Richard huku umati wa watu waliokuwa nje wakiomba atolewe ili wamfundishe adabu.





“Baadaye ukafikiwa uamuzi kuwa, wamfungie baba kwenye chumba hicho kisha wamchukue binti, wampeleke kituo cha polisi cha Kimara, Rombo ili akatoe maelezo,” alisema shuhuda huyo.

POLISI WATINGA ENEO LA TUKIO
Chanzo chetu kilizidi kutiririka kuwa, baada ya binti huyo kufikishwa kituoni na kutoa maelezo, polisi walilazimika kwenda eneo la tukio kwa lengo la kumchukua mtuhumiwa.

“Walipofika walikuta umati wa watu waliokuwa na jazba, walikuwa wakimtaka mtuhumiwa wamchome moto.

“Kufuatia hali hiyo, polisi walilazimika kuongeza nguvu ambapo baada ya muda walifika maafande wengine wakiwa na silaha, walipofungua chumba alichokuwemo mtuhumiwa, waliambulia patupu.





“Jamaa alishatoboa dari na kutimka huku akiwaacha watu solemba,” ilielezwa.

POLISI WASOMBA WATU
Baada ya kubaini mtuhumiwa kaingia mitini, polisi hao walimchukua mjumbe, mtoto pamoja na mama yake ambao walipelekwa kituo cha polisi Mbezi Louis kwa ajili ya mahojiano zaidi.





Mpaka paparazi anaondoka eneo la tukio, hali ilikuwa ni tete huku wananchi wakiapa kumfanyizia mwanaume huyo watakapomkamata. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...