Wednesday, August 24, 2011

Mume avaa nguo za kike kwenda kufumania



Mwanaume mmoja Adam Hashim (24) mkazi wa Mbezi Makonde jijini Dar es Salaam, amejikuta matatani kufuatia kutinga nguo za kike kwa lengo la kwenda kumfumania mkewe (hakujulikana jina).

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika Kituo cha Daladala cha Mbezi Shule, Dar ambapo mwanaume huyo alivaa khanga, hijabu huku usoni akiwa amejifunga kininja kwa lengo la kufuatilia nyendo za mkewe ili akamfumanie.

Hata hivyo, mume huyo ambaye ni dereva wa bodaboda maeneo hayo, hakufanikiwa kumtia mtegoni mkewe kwani kabla hajapanda gari kwenda kwenye tukio,  mtu mmoja alimtilia shaka kwa kumsalimia lakini hakuitika hivyo ‘msamaria mwema’ huyo akawaita askari waliokuwa doria na kumkamata.

Safari ya fumanizi iliishia hapo, mwanaume huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, kilichopo Tegeta, Dar.

Akisimulia mkasa huo kwa maafande kituoni hapo, Adam alisema kwamba, aliamua kufanya hivyo kutokana na wivu kwani kila alipotoka kazini alikuwa na tabia ya kumsikiliza mkewe dirishani ili kujua anazungumza na nani kwenye simu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...