Tuesday, August 30, 2011

JACK: MIMI NA ‘KUFULI’ MBALI MBALI



Sistaduu aliyewahi kushiriki Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dustan amefunguka kuwa, hapendelei kuvaa kufuli mara kwa mara anapokuwa kwenye mitoko yake.

Akipiga stori hivi karibuni maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Jack a.k.a Jack wa Maisha Plus ambaye emefanya freshi kwenye Filamu ya Senior Bachelor alisema ameamua hivyo kwa sababu amekuwa akikosa uhuru anapovaa vazi hilo.

Alisema, huko nyuma alikuwa anavaa lakini siku za hivi karibuni zimekuwa zikimletea matatizo ikiwa ni pamoja na kumsababishia muwasho sehemu zake muhimu.

“Kiukweli mimi na makufuli tuko mbali mbali, siyo kwamba kuna lingine au nataka kuwatega wanaume, hapana! Nikivaa zinaniletea muwasho na hili joto sasa ndiyo usiseme,” alisema Jack.

Jack anaungana na mastaa wengi ambao waliwahi kukiri kutovaa makufuli wanapokwenda ‘out’ huku kila mmoja akitoa sababu zake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...