Thursday, August 25, 2011

MWANAMKE ABEBWA MTUPU KWENYE BAISKEL

Mwanamke mmoja  mkazi  wa  Kata  ya Isevya iliyopo Manispaa  ya Tabora mkoani hapa, hivi karibuni alijikuta akikumbwa na aibu ya mwaka baada  ya  kuvuliwa nguo zote na kubaki kama alivyozaliwa kisha kupakizwa kwenye baiskeli.

Tukio hilo la udhalilishaji lilitokea Augosti 23, mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku katika moja ya barabara za manispaa hiyo ambapo mwanamke huyo alionekana akizozana na mwanaume mmoja kabla ya kufikia hatua ya kuachwa mtupu.

Shuhuda wa tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake aliliambia Uwazi kuwa, awali walimuona mwanamke huyo akizozana na mwanaume mmoja aliyekuwa naye lakini ghafla njemba huyo alimvua nguo kisha akaondoka nazo.





“Sisi tuliwaona wakipandishiana, haikuchukua muda mrefu mwanaume yule akaanza kumvua nguo kisha akamuacha akiwa kama alivyozaliwa, hatukujua kama ni wapenzi ama laa ila inavyoonekana wanajuana,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:

“Baadaye walitokea watu waliokuwa na baiskeli, wakamuuliza kilichomsibu, jina lake na mwanaume aliyemfanyia hivyo lakini alikataa kutaja badala yake akaomba apelekwe kwake maeneo ya Isevya Sokoni, ndipo wanaume hao walimuonea huruma na kumpa lifti akiwa mtupu hadi kwake.”

Ikaelezwa kuwa, akiwa katika usafiri huo kuelekea nyumbani kwake, watu  waliokuwa kando ya barabara walipigwa na butwaa kumuona mwanamke huyo akiwa katika mazingira hayo hali iliyowafanya baadhi yao kumhusisha na wale wanaofanya biashara ya uchangudoa.

Baadhi ya mashuhuda walilitupia lawama jeshi la polisi linaloongozwa na IGP Said Mwema kuwa hivi sasa limeacha kufanya doria na kusababisha udhalilishaji huo na hata wizi wa kutumia nguvu kufanyika hasa nyakati za usiku.

Jitihada za kumpata mwanamke huyo kuzungumzia kilichompata ziligonga mwamba kutokana na taarifa kuwa, baada ya tukio hilo alikuwa hatoki nje kukwepa aibu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...