Sunday, August 14, 2011

BHOKE, ELNEST LIVE!!!



Washiriki wa Shindano la BBA Amplified 2011, Bhoke Egina wa Tanzania na Ernest wa Uganda, hivi karibuni walinaswa laivu wakiwa katika pozi la ‘one love’.

Mastaa hao walibambwa juzikati jijini Johannesburg, Afrika ya Kusini kulikokuwa na fainali ya mashindano hayo ambapo Ernest na Bhoke walikuwa miongoni mwa waliohudhuria.

Chanzo chetu kilichokuwa eneo la tukio kilichoomba hifadhi ya jina kilifunguka: “Katika zoezi la kupiga picha mbali na kupiga na washiriki wengine, Bhoke alijipeleka kwa Ernest na kupozi mbele ya kamera katika mapozi yaliyoashiria kuwepo kwa penzi kati yao.

“Wanaonekana kupendana kwa dhati na ingekuwa mimi ningewashauri waoane ili wajiachie kwa raha zao.”
Ernest na Bhoke, hivi karibuni walipamba vichwa vya habari vya magazeti baada ya Mganda huyo kumtia doa dada yetu kwa kufanya naye mapenzi hadharani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...