Tuesday, August 30, 2011

UWOYA AMLIPUA WEMA

SUPASTAA ‘sexiest’ katika chimbo la muvi za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Oprah’ ‘amemlipua laivu’ mwigizaji mwenzake, Wema Isaac Sepetu akisema kuwa hamfikii kwa lolote...

Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii baada ya wawili hao kushindanishwa na prisenta wa Clouds TV na Radio, Zamaradi Mketema (pichani) kupitia ‘blogi’ yake ambapo wasomaji wa mtandao huo walipiga kura za kuonesha ni nani mkali wa kuigiza kati ya Uwoya na Wema.

UWOYA AIBUKA KINARA, AMFUNGUKIA WEMA
Baada ya mchakato wa upigaji kura uliochukua wiki moja kukamilika, Jumatatu ya Agosti 23, mwaka huu, Zamaradi alimtangaza Uwoya kumfunika vibaya Wema na matokeo hayo yakawekwa hewani kupitia ‘segimenti’ ya Muvi Leo kwenye Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Clouds FM.

Uwoya ambaye ni kinara wa Muvi za Oprah na Mid Night alipopigiwa simu na Zamaradi ili kusikia ‘komenti’ zake, ndipo akamfungukia Wema:

“Nilitegemea kushinda kwani Wema ni mdogo sana kisanaa, hata kama ingetokea akashinda, basi ingekuwa ndoto ya alinacha.





“Ukweli ni kwamba kwa hapa Bongo sijaona staa wa kike mwenye uwezo wa kushindanishwa na mimi.

“Ninaweza kuvaa uhusika wa aina zote tofauti na Wema ambaye ana sauti ya kitoto sana na ‘inam-limit’ kucheza baadhi ya sehemu. Anachoweza Wema ni kucheza sehemu za majonzi na mapenzi tu, lakini siyo zile za kufoka kama mimi ambaye ukinipa ‘scene’ yoyote nakamua bila tatizo. Hata sauti yake ni ya kitotototo.”

WEMA AJIBU MAPIGO
Hata hivyo, siku iliyofuata (Jumanne), Wema alipoulizwa juu ya maneno ya Uwoya alikuja juu na kujibu mapigo kwamba, yeye ndiye aliyeanza kuingia kwenye tasnia hiyo na uwezo wake ni mkubwa kuliko Uwoya.

Wema, kinara wa Filamu za White Maria na Saturday Morning alisema:  “Uwezo wangu unafahamika, huyo Uwoya asiseme kwamba anaweza kunizidi kwa kuwa amecheza muvi nyingi kuliko mimi.

“Nafikiri kuna kitu Uwoya hafahamu. Mimi ni mkali lakini sijacheza filamu nyingi. Yeye ameonekana kwa sababu amecheza filamu nyingi na baadhi ya waigizaji kama Ray (Vincent Kigosi) ambaye mimi sijabahatika kucheza naye.

“Naamini kabisa kwamba namfunika Uwoya kwa sababu naweza kutumia lugha za kimataifa kuliko yeye. Asikwambie mtu, najua ‘kimombo’ kuliko msanii mwingine yeyote hapa Bongo.”

NI VITA YA WAKUBWA
Kwa mujibu wa maoni ya wadau waliotembelea mtandao wa mtangazaji huyo, shindano hilo limeibua vita ya wakubwa kwani wote ni mastaa wenye majina makubwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...