Thursday, August 25, 2011

Demu afanya kioja cha mwaka

Mwanamke mmoja ‘demu’ ambaye jina lake halikupatikana mara moja (pichani), amegeuka kioja cha mwaka baada ya kuibuka kituo cha daladala na kufanya vituko vilivyowaacha watu midomo wazi, Ijumaa linakupa kitu ‘laivu’ bila chenga.




Tukio hilo la aina yake lilichukua nafasi katika Kituo cha Daladala cha Kanisani Kinondoni, Dar es Salaam Jumatano wiki hii majira ya saa 2:00

asubuhi ambapo mrembo huyo ‘kijeba’ aliibuka akiwa ‘ametupia’ kinguo kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maungo nyeti ya mwili wake (angalia picha za juu ukurasa wa mbele).
ALIPITIWA MUDA KURUDI NYUMBANI?
Katika ‘iventi’ hiyo iliyoshuhudiwa na Paparazi wetu, mrembo huyo alionekana kama aliyepitiwa muda wa kurejea nyumbani na alikuwa akitokea ‘kiwanja’ kujirusha.

Huku akiwa hana chembe ya aibu, mwanamke huyo alionekana akikata mitaa bila kujali kadamnasi iliyokuwa ikisubiria daladala kuwahi kazini.





WANAUME WAKWARE WAMZINGIRA
Baadhi ya wanaume wakware walimiminika na kuanza kumzingira huku wakimzomea lakini mdada huyo hakuonekana kujali chochote zaidi ya kuongeza madoido ya kutembea.

AWASHA SIGARA, AIVUTA HADHARANI
Katika kuwakata ‘ngebe’ wanaume hao na kuwadhihirishia kuwa hana mshipa wa aibu, mwanamke huyo alichomoa sigara kisha akaiwasha na kuanza kukandamiza bila kujali sheria ya uvutaji na onyo kuwa ni hatari kwa afya yake.





Wakati akiendelea kupuliza sigara kama treni ya mkaa, demu huyo alipiga ‘biti’ mwanaume kumsogelea kwa madai kwamba atamfanyia kitu mbaya.

MAMA WA MAKAMO AJITOKEZA KUMSITIRI
Katika tukio hilo, mama mmoja wa makamo (jina halikupatikana mara moja) aliyeonekana kusikitishwa zaidi na tukio hilo, alimfuata na kumuuliza anakoishi ambapo alijibu kuwa maskani yake ni Kinondoni Mkwajuni, Dar.





Katika kumsitiri, mama huyo alitoa ‘ngawira’ za Kibongo Shilingi 3,000 akamkabidhi na kumtaka achukue teksi imkimbize nyumbani.

Cha kushangaza, mrembo huyo alichukua fedha hizo akazama kwenye kibanda kimoja kilichopo kituoni hapo kisha akanunua ‘kiroba’ cha pombe kali na sigara akaanza kuvizamisha mwilini huku akidai kuwa alikuwa na kiu ya ‘kufa mtu’.





ATAKA KIDUME WA KUONDOKA NAYE
Vituko vya mrembo huyo havikuishia hapo kwani wakati ‘akigida’ kiroba,

alitaka ajitokeze kidume mmoja ili aambatane naye nyumbani kwake akamwoneshe kwamba yeye ni mwanamke wa shoka (bila kusema atakachokwenda kumfanyia).





ACHIMBA MKWARA, AINGIA UCHOCHORONI
Wakati ‘akifotolewa’ picha, alisikika akichimba mkwara kwamba endapo picha zake zitatumika gazetini au mahali popote, atamtoa mtu ‘mshipa’.

Alipofuatwa na Paparazi wetu kwa mahojiano, mwanamama huyo alikuwa na haya ya kusema:





“Kwani wewe unanifahamu? Ole wako ukinitoa gazetini, Mungu wangu nitakufanyia kitu ambacho hutasahau hadi unakwenda ahera. Utanitafuta kuniomba msamaha ukiwa unatambaa.”

Alisema binti huyo akiingia uchochoroni na kupotelea kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...