Tuesday, August 2, 2011

Haina MAJOTROOOO....


Staa wa Hip Hop duniani, Christopher Brian Bridges ‘Ludacris’, jana alfajiri alithibitisha kuwa kila anapoweka maguu yake amani hutoweka, alichokifanya kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam ni full balaa.


Luda a.k.a Chris Lova Lova, alitanguliwa na DJ wake aliyeanza kufanya maunjanja na baadaye mwenyewe alipopanda, hali ya hewa ilibadilika.

Mchizi huyo ambaye ni mmiliki wa lebo ya Disturbing tha Peace (usumbufu wa amani), alitii kiu ya kila shabiki wa burudani aliyehudhuria tukio la Fiesta 2011 kutokana na mzigo wa kiwango cha juu alioufanya jukwaani.



Watangazaji wenye majina makubwa Bongo, Adam Mchomvu, Hamis Mandi ‘B12’ na Fatma Hassan walitangulia kuwaandaa mashabiki kabla ya mtu mzima Luda kutinga jukwaani.
Mbali na Luda, shoo hiyo ilitikisa kutokana na burudani ya aina yake iliyoporomoshwa na na wasanii mbalimbali wa Kibongo.

MATUKIO MENGINE YALIYOJIRI
Brazameni Abdul Sykes ‘Dully’ alipanda jukwaani saa 6:00, lakini makeke yake yaliishia kwa sauti kukwama baada ya kuishiwa pumzi.


Hata hivyo, mtindo wa kuimba juu ya wimbo (Playback) ilimuokoa kwani sauti yake ilishaanza kupotea kutokana na kuishiwa na pumzi.

Hata hivyo, alijitahidi kuonesha uwezo. Dully alitarajiwa pia kugonga shoo jana jioni kwenye sherehe ya Fainali ya Big Brother Amplified nchini Afrika Kusini.



WAKONGWE WA BONGO FLEVA WAENZIWA
Licha ya swaga za kila aina zilizokuwepo, Clouds Media pia waliandaa tuzo za heshima ambapo Kundi la East Coast, Man Dojo na Domo Kaya, Dully Sykes, Juma Nature, Profesa Jay, Mr Nice, Lady Jay Dee, Unique Sisters, Bushoke, Fid Q  walipewa tuzo kwa mchango wao katika miaka 10 ya Fiesta.


ROMA AMTAJA PROFESA JAY ZAIDI YA MARA 10
Kituko kingine kilikuwa ni wakati wa kukabidhi tuzo za heshima ambapo wasanii wapya walipewa heshima ya kuwakabidhi wakongwe. R.O.M.A alipewa nafasi ya kumkabidhi Profesa Jay lakini kabla ya kufanya makabidhiano, alianza kwa kumpamba kinoma.
Kuonyesha ni kwa kiasi gani anamkubali, alitaja majina yake ya kisanii zaidi ya kumi.


BOB JUNIOR ATOA KALI
Bob Junior alipopanda jukwaani alijinadi: “Mimi ni Rais wa Masharobaro lakini Mr Nice ni Rais wa Viuno.” Kauli hiyo ilipokelewa tofauti na mashabiki waliokuwa wamejaa viwanjani hapo.




BLU APANDA JUKWAANI AKIWA TILA LILA
Herry Samir ‘Blu’ alipanda jukwaani akiwa tayari yuko bwii. Kama jina la wimbo wake mpya lilivyo, jamaa alipanda akiwa tilalila na kushindwa kuonesha kile ambacho mashabiki wake walikitegemea. 



KIVAZI CHA LINAH DUH!
Msanii kutoka Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Estelina Sanga alikuwa kituko kutokana na kivazi alichokuwa amevaa. Alipanda jukwaani kukabidhi tuzo kwa Lady Jay Dee ambayo ilipokelewa na mume wa mkongwe huyo wa Bongo Fleva, Gardiner G. Habash.


Mashabiki walipiga mayowe wakimtaka ageuke waone makalio yake yaliyokuwa yakionekana kutokana na kivazi alichokuwa ametinga.




Linah akilikata ndani ya FIESTA...




BUSHOKE AZOMEWA
Mambo hayakuwa mazuri kwa Bushoke kwani alipoitwa jukwaani kupewa tuzo ya heshima kisha kupewa mic, alianza kuzungumzia siasa huku akiwapa shavu vigogo kadhaa serikalini, jambo lililoonesha kuwakera mashabiki.
Alipoendelea mashabiki walianza kumzomea na kumtaka ashuke. Kuua soo ikabidi jamaa atereke kwa unyonge...

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...