Tuesday, August 30, 2011
MACHANGU WALIA NJAA
Safari ya blog hii kuwatembelea machangudoa wa jijini Dar es Salaam ilikamilika kwa kukusanya kilio chao kikubwa ambapo ilibainika wote wanalia hali ya ukame iliyopo sasa, mistari inayofuata inakupa ‘eibisii’.
Hivi karibuni, kikosi kamili cha wapiga picha wetu walitia timu sehemu mbalimbali za jiji ambazo makahaba wanatega wanaume lengo likiwa ni kujua wanachozungumza katika kipindi hiki cha mfungo.
Wengi walisema hali ni ngumu kiasi cha kukatisha tamaa na mbaya zaidi, wengi wao wanapotoka majumbani usiku kuelekea kwenye ‘lindo’ hubeba nauli ya kuendea tu wakiamini watarudi na Bajaj baada ya kunasa wateja.
Prisca Makungu, kahaba anayepatikana maeneo ya Kinondoni, Dar alisema kuwa zamani alikuwa akikamata shilingi elfu 90 kwa wiki lakini kwa sasa siku saba zinakatika akiwa na shilingi elfu ishirini tu mkononi.
Anna Singano, ni kahaba Corner Bar, Sinza. Anasema kwa sasa anaweza kukata wiki moja bila kuweka kibindoni hata shilingi elfu 10, wakati mwingine anakopa nauli kwa madereva wa Bajaj wa eneo hilo ili aweze kurudi nyumbani kwake, Mabibo.
Isha Suzu, kahaba nje ya Ukumbi wa Sun Cirro, uliopo Shekilango, Ubungo jijini Dar anasema hali ni mbaya. Anafikiria kutafuta kazi za ndani ‘uhausigeli’ ili aweze kujikwamua kimaisha.
Mwajabu Idi, anauza mwili maeneo ya Keys Hotel, Mnazi Mmoja, Dar. Anasema katika kipindi hiki kigumu kwa biashara amelazimika kuchagua siku za kwenda ‘kazini’.
“Hali mbaya jamani. Mimi nimeamua kuchagua siku za kuja, kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili nakuja, baada ya hapo nalala tu kwani hata nikija sipati ‘pesa’ za kunitosheleza kama zamani.
Katika hali ya kustaajabisha, kahaba mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Rehema alianika kwamba, katika kipindi hiki cha ukame wa wanaume wakware, wanalazimika kuwapunguzia wateja kiwango cha mshiko.
“Kabla ya hali hii ngumu, mwanaume akitaka kuondoka na mimi lazima anipe shilingi elfu 20 keshi, siku hizi hadi elfu 5 napokea, nitafanyaje sasa?” alihoji Rehema.
Kahaba mwingine, mwanadada mtu mzima aliyekutwa na gazeti hili pembeni ya kituo cha mafuta maeneo ya Sinza Mori alisema katika kipindi hiki cha ukame, wasichana ndiyo wanaondoka kidedea.
“Mimi leo nimeingia hapa (kazini) saa nne usiku, lakini mpaka muda huu (saa saba) sijamwona mwanaume wa kuniongelesha. Hawa machangu wadogo ndiyo wanakula nyomi,” alisema kahaba huyo aliyedai anaitwa Dija mwenye umri wa miaka 41.
KUTOKA KWA MHARIRI;
Wito wa gazeti hili ni kwa serikali kuweka mazingira ambayo yatawasaidia hawa akina dadapoa wanaoishi kwa kutegemea biashara ya kuuza miili wafanye kazi nyingine.
Hii pia itasaidia kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo utafiti unaonesha kuwa, ukahaba nao unachangia.
UWOYA AMLIPUA WEMA
SUPASTAA ‘sexiest’ katika chimbo la muvi za Kibongo, Irene Pancras Uwoya ‘Oprah’ ‘amemlipua laivu’ mwigizaji mwenzake, Wema Isaac Sepetu akisema kuwa hamfikii kwa lolote...
Tukio hilo lilijiri mwanzoni mwa wiki hii baada ya wawili hao kushindanishwa na prisenta wa Clouds TV na Radio, Zamaradi Mketema (pichani) kupitia ‘blogi’ yake ambapo wasomaji wa mtandao huo walipiga kura za kuonesha ni nani mkali wa kuigiza kati ya Uwoya na Wema.
UWOYA AIBUKA KINARA, AMFUNGUKIA WEMA
Baada ya mchakato wa upigaji kura uliochukua wiki moja kukamilika, Jumatatu ya Agosti 23, mwaka huu, Zamaradi alimtangaza Uwoya kumfunika vibaya Wema na matokeo hayo yakawekwa hewani kupitia ‘segimenti’ ya Muvi Leo kwenye Kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na Clouds FM.
Uwoya ambaye ni kinara wa Muvi za Oprah na Mid Night alipopigiwa simu na Zamaradi ili kusikia ‘komenti’ zake, ndipo akamfungukia Wema:
“Nilitegemea kushinda kwani Wema ni mdogo sana kisanaa, hata kama ingetokea akashinda, basi ingekuwa ndoto ya alinacha.
“Ukweli ni kwamba kwa hapa Bongo sijaona staa wa kike mwenye uwezo wa kushindanishwa na mimi.
“Ninaweza kuvaa uhusika wa aina zote tofauti na Wema ambaye ana sauti ya kitoto sana na ‘inam-limit’ kucheza baadhi ya sehemu. Anachoweza Wema ni kucheza sehemu za majonzi na mapenzi tu, lakini siyo zile za kufoka kama mimi ambaye ukinipa ‘scene’ yoyote nakamua bila tatizo. Hata sauti yake ni ya kitotototo.”
WEMA AJIBU MAPIGO
Hata hivyo, siku iliyofuata (Jumanne), Wema alipoulizwa juu ya maneno ya Uwoya alikuja juu na kujibu mapigo kwamba, yeye ndiye aliyeanza kuingia kwenye tasnia hiyo na uwezo wake ni mkubwa kuliko Uwoya.
Wema, kinara wa Filamu za White Maria na Saturday Morning alisema: “Uwezo wangu unafahamika, huyo Uwoya asiseme kwamba anaweza kunizidi kwa kuwa amecheza muvi nyingi kuliko mimi.
“Nafikiri kuna kitu Uwoya hafahamu. Mimi ni mkali lakini sijacheza filamu nyingi. Yeye ameonekana kwa sababu amecheza filamu nyingi na baadhi ya waigizaji kama Ray (Vincent Kigosi) ambaye mimi sijabahatika kucheza naye.
“Naamini kabisa kwamba namfunika Uwoya kwa sababu naweza kutumia lugha za kimataifa kuliko yeye. Asikwambie mtu, najua ‘kimombo’ kuliko msanii mwingine yeyote hapa Bongo.”
NI VITA YA WAKUBWA
Kwa mujibu wa maoni ya wadau waliotembelea mtandao wa mtangazaji huyo, shindano hilo limeibua vita ya wakubwa kwani wote ni mastaa wenye majina makubwa.

JACK: MIMI NA ‘KUFULI’ MBALI MBALI
Sistaduu aliyewahi kushiriki Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dustan amefunguka kuwa, hapendelei kuvaa kufuli mara kwa mara anapokuwa kwenye mitoko yake.
Akipiga stori hivi karibuni maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Jack a.k.a Jack wa Maisha Plus ambaye emefanya freshi kwenye Filamu ya Senior Bachelor alisema ameamua hivyo kwa sababu amekuwa akikosa uhuru anapovaa vazi hilo.
Alisema, huko nyuma alikuwa anavaa lakini siku za hivi karibuni zimekuwa zikimletea matatizo ikiwa ni pamoja na kumsababishia muwasho sehemu zake muhimu.
“Kiukweli mimi na makufuli tuko mbali mbali, siyo kwamba kuna lingine au nataka kuwatega wanaume, hapana! Nikivaa zinaniletea muwasho na hili joto sasa ndiyo usiseme,” alisema Jack.
Jack anaungana na mastaa wengi ambao waliwahi kukiri kutovaa makufuli wanapokwenda ‘out’ huku kila mmoja akitoa sababu zake.
KUKU ATOA UHAI WA MTU
MAREHEMU NASIB EXZAVERY maalufu kama Mkemia akiwa amechomwa moto eneo la viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya kwa kosa la wizi wa kuku ambaye Mwenye Kuku huyo hajafahamika.
Nasib Xavery, maarufu kama Mkemia jana aliuawa na wananchi wenye hasira kwa kuchomwa moto katika eneo la Shule ya Msingi Mwenge, jijini Mbeya, kutokana na kile kilichodaiwa kuiba kuku.
Sunday, August 28, 2011
HATARI...
MAPENZI kutoka moyoni ni simulizi kwa mastaa wengi Bongo, nyanyuka nikae ndiyo zao kama kupishana siti za daladala, mtindo ni kujihudumia a.k.a self service.
Mtindo wa kuzungukana na kuchukuliana wapenzi na wachumba siyo stori kwao, warembo kadhaa wameshakutana kwa wanaume zaidi ya mmoja na kuchangia penzi, wakanuniana kwanza, baadaye urafiki wa mashaka ukaendelea.
AUNT NA WEMA
Staa wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ na Miss Tanzania 2006-07, Wema Isaac Sepetu wanadaiwa kukutana kwenye penzi la mjasiriamali maarufu Bongo, Jack Pemba.
Pamoja na madai hayo, Wema amekuwa akikanusha kutoa penzi kwa Pemba ingawa vyanzo vya habari vinasisitiza.
Kwa sasa, Pemba ambaye aliigiza na Aunt katika filamu ya Miss Bongo, amejinasua kwenye mapenzi na warembo maarufu, hivi sasa ametulia na mwenzi wake ambaye hana jina kubwa mjini.
Aunt na Wema, pia walikutana kwenye penzi la Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Hartmann Mbilinyi ambaye kuna kipindi alinusurika kuugua uchizi kwa mapenzi ya warembo wauza ‘nyago’ kwenye filamu.
AUNT NA SARA
Aunt anaendelea kutengeneza ‘paragrafu’, kwani anatuhumiwa kuingia kwenye anga za muigizaji mwenzake, Sara Mwakapala ‘Bukabi’ na kumchukulia mchumba wake, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’.
Sara alidai kumfumania Aunt chumbani akiwa na Silva, baada ya hapo mrembo huyo alibaki na ujauzito ambao ameshajifungua, huku baba wa mtoto akiendelea kujidai na Gwantwa.
JACK PENTZEL NA WEMA
Staa mwenye ‘kashkashi’ za wanaume, Jacqueline Pentzel anadaiwa kukutana na Wema kwenye penzi la muigizaji maarufu Bongo, Jumanne Kihangala ‘Mr. Chuz’.
Kwa awamu hiyo, Wema anakanusha kutoka kimapenzi na Chuz, ingawa vyanzo vinasisitiza ukweli wa data zenyewe.
Jack na Wema ambao wanajidai ni marafiki wakubwa, wanadaiwa kukutana kwenye penzi la staa wa African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel Mbwana ‘Charlz Baba’ ambaye ni mzazi mwenza wa mshindi namba mbili wa Kimwana Manywele 2007, Husna Idd ‘Sajent’.
Hata hivyo, kwa hapa Jack ndiye anakunusha, ingawa ameshindwa kujitoa kwenye skendo hiyo.
KIRUNGU CHA MR. CHUZ
Wema na Jack siyo peke yao ambao wamo kwenye orodha, wasanii wenye majina makubwa Bongo, Miriam Jolwa ‘Kabula’, Joan Matovolwa na Leila Ismail ‘Lily’ kwa nyakati tofauti pia wamepitiwa na kirungu cha Mr. Chuz.
WEMA NA WOLPER
Hivi sasa Wema anaweka wazi kwamba amejituliza kwa mkali wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ lakini janki huyo huyo amesharipotiwa kuchakachua na nyota wa filamu, Jacqueline Wolper.
Mshiriki wa Miss Kiswahili, Rehema Fabian naye ameshajitangaza kuwahi kutoka kimapenzi na Diamond kama ilivyo kwa mshiriki wa Shindano la Maisha Plus Season II, Upendo Moshi.
MAINDA NA JOHARI
Mastaa wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ na Ruth Suka ‘Mainda’, wao siyo stori kwamba wamekuwa ‘wakinyang’anyia’ penzi la galacha wa sanaa za maigizo nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Kwa upande mwingine, Ray ameshahusishwa kutoka kimapenzi na mtangazaji maarufu Bongo, Joyce Kiria ingawa hakuna mmoja kati yao aliyewahi kujitokeza kupinga wala kukubali.
UWOYA NA JACK PATRICK
Staa wa filamu, Irene Uwoya Ndikumana ‘Mama Krish’ kabla hajafunga ndoa anadaiwa kuchangia penzi na Miss Ilala namba tatu 2005, Jacqueline Patrick ‘Jack wa Chuz’.
Mwanaume aliyedaiwa kuwagonganisha ni dalali wa magari, Ifraj Haroub ambaye ni mtoto wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Koani, Haroub Masoud.
Ifraj, alisharipotiwa kutoka kimapenzi na mshiriki wa Miss Tanzania 2011, Husna Maulid, ikiwa ni pamoja na picha zao ‘wakichakachua’ dhambi ya zinaa kuanikwa.
UWOYA NA QUEEN SUZY
Skendo ilivuma kwamba Uwoya akiwa ndani ya ndoa, pia alitoka kimapenzi na nguzo ya Bendi ya Mapacha Watatu, Kalala Hamza ‘Kalala Junior’.
Ishu hiyo, ilisababisha ugomvi kati ya staa huyo wa filamu na aliyekuwa mchumba wa Kalala, Mary Junior ambao ulitimka Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam.
Kashfa hiyo, inakwenda mbali zaidi na kuzalisha tawi kwamba Uwoya aliwahi kuchangia penzi na mnenguaji Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ anayedai amezaa na Kalala ambaye anamkana mtoto.
UWOYA NA FLORA
Uwoya amewahi kutoka kimapenzi na mwanamuziki Hamis Baba ‘H Baba’ ambaye kwa sasa amejituliza kwa msanii wa filamu, Flora Mvungi.
KAJALA NA RAY C
Muigizaji Kajala Masanja amewahi kuripotiwa kupigana na mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, wakigombea penzi la prodyuza maarufu wa Bongo Fleva, Paul Matthysse ‘P Funk’.
Kajala ni mzazi mwenzake P Funk, wakati Ray C baada ya hapo alijiweka kwa staa wa Big Brother, Mwisho Mwampamba kabla ya kutua kwa memba wa Kundi la Nako 2 Nako, Isaac Waziri Makuto lakini wote walishamwagana.
SYLVIA, LISA, NARGIS
Mamis Ilala, Nargis Mohamed (2003) na Sylvia Shally (2009), Miss Tanzania namba 3 2006, Lisa Jensen na muigizaji, Shamsa Ford wamewahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘taikuni’ wa Bongo Movie, Steven Kanumba. Hata hivyo, Lisa anakanusha.
Friday, August 26, 2011
SHINDANO LA AIBU
Mijimama miwili, Mwajuma Thabit ‘Rose Jimama’ (kushoto) na Fransisca Mbena ‘Chuma’ hivi karibuni ilinaswa na paparazi wetu ikishindana kuwa nani ana makalio makubwa kuliko mwenzake bila kujali watu waliokuwa wakiwakodolea macho.
Mijimama hiyo ilikutwa na paparazi wetu ikifanya kufuru hiyo Jumapili ya Agosti 21, mwaka huu nje ya nyumba moja iliyopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wapita njia walipowaona wanawake hao ambao ni wake za watu, wengine walifurahia huku baadhi wakionesha sura za kushangaa na kuhoji, kulikoni watu wazima kama hao kufanya vitendo vya ovyo?
Kufuatia tukio hilo, mpigapicha wetu alizungumza na mmoja wao ambaye alisema walikuwa kwenye maandalizi ya shindano la Mwanamke Nyonga linalotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Iddi Pili.
Jimama hilo lilisema wameanza mazoezi mapema baada ya kusikia kuwa, katika mpambano huo kutakuwa na mijimama mingine iliyokubuhu kwenye masuala ya unyago, hususan mambo ya nyonga.
“Tumeamua kufanya mazoezi mapema kwa kuwa tumesikia wenzetu tunaokwenda kushindana nao ni mijimama ya nguvu na mambo yao si mchezo,” alisema Mwajuma.
Thursday, August 25, 2011
MWANAMKE ABEBWA MTUPU KWENYE BAISKEL
Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Isevya iliyopo Manispaa ya Tabora mkoani hapa, hivi karibuni alijikuta akikumbwa na aibu ya mwaka baada ya kuvuliwa nguo zote na kubaki kama alivyozaliwa kisha kupakizwa kwenye baiskeli.
Tukio hilo la udhalilishaji lilitokea Augosti 23, mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku katika moja ya barabara za manispaa hiyo ambapo mwanamke huyo alionekana akizozana na mwanaume mmoja kabla ya kufikia hatua ya kuachwa mtupu.
Shuhuda wa tukio hilo aliyeomba hifadhi ya jina lake aliliambia Uwazi kuwa, awali walimuona mwanamke huyo akizozana na mwanaume mmoja aliyekuwa naye lakini ghafla njemba huyo alimvua nguo kisha akaondoka nazo.
“Sisi tuliwaona wakipandishiana, haikuchukua muda mrefu mwanaume yule akaanza kumvua nguo kisha akamuacha akiwa kama alivyozaliwa, hatukujua kama ni wapenzi ama laa ila inavyoonekana wanajuana,” alisema shuhuda huyo na kuongeza:
“Baadaye walitokea watu waliokuwa na baiskeli, wakamuuliza kilichomsibu, jina lake na mwanaume aliyemfanyia hivyo lakini alikataa kutaja badala yake akaomba apelekwe kwake maeneo ya Isevya Sokoni, ndipo wanaume hao walimuonea huruma na kumpa lifti akiwa mtupu hadi kwake.”
Ikaelezwa kuwa, akiwa katika usafiri huo kuelekea nyumbani kwake, watu waliokuwa kando ya barabara walipigwa na butwaa kumuona mwanamke huyo akiwa katika mazingira hayo hali iliyowafanya baadhi yao kumhusisha na wale wanaofanya biashara ya uchangudoa.
Baadhi ya mashuhuda walilitupia lawama jeshi la polisi linaloongozwa na IGP Said Mwema kuwa hivi sasa limeacha kufanya doria na kusababisha udhalilishaji huo na hata wizi wa kutumia nguvu kufanyika hasa nyakati za usiku.
Jitihada za kumpata mwanamke huyo kuzungumzia kilichompata ziligonga mwamba kutokana na taarifa kuwa, baada ya tukio hilo alikuwa hatoki nje kukwepa aibu.

MTOTO ALIYEISHI NA NYANI AFANYA MAAJABU
MTOTO Baraka Bahati Rose (14), (pichani) aliyeishi na nyani porini kwa kipindi cha miaka mitano na kuokolewa na maofisa wanyama pori, amebadilika na sasa anaonesha maajabu katika kusakata soka na pia kufanya vizuri darasani.
Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Kimanga, Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Christina, aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa Baraka amekuwa akifanya vizuri na kucheza mpira kitaalamu zaidi, hali inayomfanya apendwe na walimu na wanafunzi.
“Baraka anajitahidi sana na siyo katika masomo tu bali hata katika mchezo wa mpira wa miguu, ni staa na anapenda kujisomea, amekuwa akifanya vizuri sana hasa katika masomo ya Sayansi,” alisema Mwalimu Chris.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliliambia gazeti hili kwamba, Baraka ambaye yupo Darasa la Nne kwa sasa amebadilika kwa asilimia kubwa katika masomo ya Sayansi na amekuwa akicheza mpira wa miguu vizuri kuliko wenzake.
“Tunapocheza mpira wa miguu na kuchagua timu, kila mtu anapenda awe katika timu yake,” alisema mtoto mmoja wa kiume aliyejitambulisha kwa jina la Said.
Wanafunzi hao walisema kuwa Baraka amekuwa akiwapenda wenzake tofauti na awali ambapo alikuwa haongei vizuri Kiswahili na hakuwa na uhusiano mzuri na wanafunzi wengine.
Mtoto Baraka aliokolewa na maafisa wanyama pori miaka kadhaa iliyopita katika pori la Usangu, Wilaya ya Bukombe, Shinyanga baada ya askari hao kumuua nyani aliyekuwa akimtunza porini.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga, Pastor Kyombia kwa kushirikiana na mlezi wa Baraka aitwaye Rose Mbwambo wamekuwa wakimtunza mtoto huyo.

SIKU FACEBOOK IKIFUNGWA, BALAA LAKE HILI HAPA!
IRENE ANDERSEN MWANAMAMA MTUNISHA MISULI ANAYEOGOPEKA
IRENE ANDERSEN ni mwanamama aneyetisha katika utunishaji misuli kutoka nchini Sweden.
Ni mwanamke anayetisha kwa sababu mchezo huu wa kutunisha misuli umezoeleka kuwa ni kwa ajili wa wanaume tu. Inashangaza kuona mwanamama mwenye misuli mikubwa kama Irene.
Mchezo wa kutunisha misuli kwa akina mama ulianza mwishoni mwa miaka ya 1970 ambapo wanawake walianza kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya utunishaji misuli. Irene ni mmoja wa waanzilishi wa mchezo huo.
Irene alizaliwa Denmark mwaka 1966, baadaye alihamia Sweden akiwa na umri wa miaka miwili pamoja na wazazi wake.
Alikulia Malmo na baadaye kuhamia Gothenburg wakati akiwa na umri wa miaka 20. Amekuwa akitumia muda wake mwingi katika 'gym' akifanya mazoezi makali ili kujenga mwili wake huu wa maajabu.
Irene mwenyewe alikuwa na haya ya kusema: "Nimekuwa nikijifunza maisha yangu yote... Wakati nikiwa mdogo, nilianza na jazz ballet na judo na nilipokuwa na umri wa miaka 15 ndipo nilipoanza mchezo wa kutunisha misuli.
Rafiki yangu alikuwa anamiliki gym na ndiye aliyenifanya niupende sana mchezo huu. Tangia hapo, nimekuwa nikifuatilia kila kitu kinachohusiana na mchezo wa kutunisha misuli kwa wanawake".
Vilevile Irene anaweza michezo ya Kick na Thai boxing, hivyo tunawashauri kutomtania mwanamama huyu pindi muwapo mitaani na mmchukulie kama wanawake wengine.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za mwanamama Irene:

‘Twanga Pepeta’
Kikosi kamili cha Bendi ya African Star International ‘Twanga Pepeta’ leo kinatarajiwa kuteremsha burudani nzito ya kukata na shoka ndani ya Ukumbi wa Mawenzi Garden Tabata jijini Dar.
Akizungumza na gazeti hili juzi, mratibu wa onesho hilo, Sauda Mwilima, ‘Top Queen’ alisema shoo ya wakali hao iliyopewa jina la ‘Usiku wa kusugua kisigino’ itakuwa kali kutokana na maandalizi yaliyofanywa hasa ukizingatia kuwa litakuwa onesho la kwanza kwa mwaka huu katika ukumbi huo.
“Hili ni onyesho la kwanza kwa wakazi wa Tabata katika mwaka huu wa 2011, kwa maana hiyo bendi imejipanga kuhakikisha inafanya makubwa na kuacha simulizi kwa wakazi wa maeneo hayo,” alisema Sauda na kuongeza kuwa kiingilio katika shoo hiyo iliyopangwa kuanza saa tatu usiku kitakuwa ni ‘buku’ tano tu.
Unamfumania mpenzi wako lakini hauko tayari kumkosa, ufanyeje?
Nimemfumania, kaamua kunipotezea
Swali:Niliwahi kuwa na mpenzi wangu lakini siku za hivi karibuni nilimfumania na rafiki yangu laivu wakiwa katika mazingira yanayoonesha kuwa walikuwa wakifanya mapenzi.
Baada ya kumnasa niliumia sana hasa kutokana na maelezo yake ya awali kwamba, angenipenda daima na kamwe asingenisaliti.
Cha ajabu baada ya tukio hilo, kutokana na kukasirishwa nikaamua kumpotezea nikijua angenitafuta na kuniomba msamaha.
Cha ajabu tangu siku hiyo na yeye akawa hana ‘taimu’ na mimi kama mtu ambaye hajuti kwa kitendo alichokifanya na wala hajuti kunikosa. Mimi nampenda sana na nahisi siko tayari kumkosa. Nimtafute nimwambie kuwa yaliyopita nimesamehe tuendelee na uhusiano wetu au nimuache tu? Nisaidie katika hili Anko.
Jibu:Kwanza kabisa kitendo alichofanya huyo mpenzi wako kinaonesha wazi kwamba, hana mapenzi ya dhati na wewe na kama utang’ang’ania kuendelea kuwa naye, ipo siku atakuja kukuumiza zaidi ya hapo.
Kama ni mtu anayekupenda, angeonesha kujutia kosa lake na hapo ningeweza kukushauri umsamehe kisha umpe nafasi nyingine lakini kama kaamua kuuchuna, sioni sababu ya wewe kumtafuta. Muache na hata kama itakuwa ndiyo moja kwa moja amini kwamba huyo hakupangwa kuwa mumeo. Wako yuko njiani.
Wivu wa mpenzi wangu
unatishia amani ya penzi letu
Swali: Anko Shalua, mpenzi wangu ana wivu sana, inafika wakati naona ni kero kwangu kwani wivu wake umepitiliza. Je, ni kweli wivu una nafasi katika mapenzi?
Je, kuna faida zozote za wivu huu ambao wakati mwingine hutishia amani ya penzi letu? Kama zipo naomba unisaidie ili nijue nisimchukie mpenzi wangu kwani huenda ana nia njema ni tatizo la mimi kutomuelewa tu.
Mohammed R.
Kibamba.
Jibu:Huko nyuma nilishawahi kuandika makala iliyokuwa inahusu wivu na nafasi yake katika mapenzi. Nikasema kwamba, wivu katika uhusiano wa dhati una nafasi kubwa na nikaongeza kuwa, endapo utaingia kwenye uhusiano na mtu na akaonesha kutokuwa na wivu kabisa na wewe, huyo penzi lake kwako litakuwa na walakini.
Hata hivyo, niseme tu kwamba kila kitu kikizidi kiwango kinakuwa na madhara, wazungu wanasema ‘everything too much is harmful’.Wivu nao ukizidi sana ni tatizo na kweli inaweza kuwa sababu ya nyie kuachana.
Kwa kifupi wivu usio wa kupitiliza una
faida kama zifuatazo;
Kwanza inaonesha kujali. Sote tunaamini pasipo na wivu hata chembe, hapana mapenzi ya dhati. Mpenzi wako anapoonesha wivu kwako anakujulisha ni kiasi gani anakujali na kukupenda na kwamba wewe ni mtu maalum sana kwake.
Jamani, mahali penye mapenzi yasiyo na wivu hata kidogo, panatia shaka! Na mara nyingi majibu yake ni kutokuwa ‘sirias’ katika uhusiano huo au huenda kuna kupitisha muda tu na kwamba labda hakuna ‘future’ na mpenzi huyo au ni dalili ya kuchuja kwa penzi.
Pili, inadhihirisha kwamba anathamini uhusiano wenu. ‘Siyo kama sikuamini mume wangu, bali wivu wangu kwako ni katika kuuthamini uhusiano wetu, mimi na wewe ni umoja wenye thamani kubwa, tusiruhusu kuuchezea nje yetu! Huu ni mfano wa ujumbe unaoonesha maana na nafasi ya wivu katika uhusiano wa kimapenzi.
Tatu, ni katika kukumbushana. Kauli au matendo yanayoashiria kumuonesha wivu mpenzio yanasaidia kwa kiasi kikubwa kumfanya asijisahau katika jukumu la kulienzi penzi lenu hata akiwa mbali ya upeo wa macho yako.
Nne, ni kujijengea heshima. Kwa namna moja au nyingine, wivu pia huweza kukujengea heshima. Kwa mfano mume mwenye wivu na mkewe hujijengea heshima ya kwamba kweli anamjali na kumpenda mkewe lakini pia anaweka mazingira ya kutosumbuliwa kwa mke wake huyo kumjengea heshima yake kama mke wa mtu.
Tano, inasaidia kubadilisha tabia. Ukiwa na wivu, unaotokana na mavazi tatanishi anayopendelea kuvaa mpenzi wako kwa mfano, huenda ikasaidia kubadili tabia yake.
“Ni kweli umependeza na umetoka ‘chicha’ ile mbaya mpenzi, lakini mh! Naogopa wanaume wakware watakusumbua honey, unaonaje ukavaa simpo tu?” Kama anakupenda huenda akabadilika kidogo na hivyo ‘vivazi vyake.
Niliyoyaeleza hapo juu ni baadhi tu ya faida za wivu.Kwa maana hiyo isifike wakati ukamchukia mpenzi wako kwa kuonesha wivu kwako. Yawezekana anafanya hivyo kwa lengo la kuboresha na si kuharibu uhusiano na kutokuelewa kwako ndiko kunakufanya uone ni kero.
Demu afanya kioja cha mwaka
Mwanamke mmoja ‘demu’ ambaye jina lake halikupatikana mara moja (pichani), amegeuka kioja cha mwaka baada ya kuibuka kituo cha daladala na kufanya vituko vilivyowaacha watu midomo wazi, Ijumaa linakupa kitu ‘laivu’ bila chenga.
Tukio hilo la aina yake lilichukua nafasi katika Kituo cha Daladala cha Kanisani Kinondoni, Dar es Salaam Jumatano wiki hii majira ya saa 2:00
asubuhi ambapo mrembo huyo ‘kijeba’ aliibuka akiwa ‘ametupia’ kinguo kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maungo nyeti ya mwili wake (angalia picha za juu ukurasa wa mbele).
ALIPITIWA MUDA KURUDI NYUMBANI?
Katika ‘iventi’ hiyo iliyoshuhudiwa na Paparazi wetu, mrembo huyo alionekana kama aliyepitiwa muda wa kurejea nyumbani na alikuwa akitokea ‘kiwanja’ kujirusha.
Huku akiwa hana chembe ya aibu, mwanamke huyo alionekana akikata mitaa bila kujali kadamnasi iliyokuwa ikisubiria daladala kuwahi kazini.
WANAUME WAKWARE WAMZINGIRA
Baadhi ya wanaume wakware walimiminika na kuanza kumzingira huku wakimzomea lakini mdada huyo hakuonekana kujali chochote zaidi ya kuongeza madoido ya kutembea.
AWASHA SIGARA, AIVUTA HADHARANI
Katika kuwakata ‘ngebe’ wanaume hao na kuwadhihirishia kuwa hana mshipa wa aibu, mwanamke huyo alichomoa sigara kisha akaiwasha na kuanza kukandamiza bila kujali sheria ya uvutaji na onyo kuwa ni hatari kwa afya yake.
Wakati akiendelea kupuliza sigara kama treni ya mkaa, demu huyo alipiga ‘biti’ mwanaume kumsogelea kwa madai kwamba atamfanyia kitu mbaya.
MAMA WA MAKAMO AJITOKEZA KUMSITIRI
Katika tukio hilo, mama mmoja wa makamo (jina halikupatikana mara moja) aliyeonekana kusikitishwa zaidi na tukio hilo, alimfuata na kumuuliza anakoishi ambapo alijibu kuwa maskani yake ni Kinondoni Mkwajuni, Dar.
Katika kumsitiri, mama huyo alitoa ‘ngawira’ za Kibongo Shilingi 3,000 akamkabidhi na kumtaka achukue teksi imkimbize nyumbani.
Cha kushangaza, mrembo huyo alichukua fedha hizo akazama kwenye kibanda kimoja kilichopo kituoni hapo kisha akanunua ‘kiroba’ cha pombe kali na sigara akaanza kuvizamisha mwilini huku akidai kuwa alikuwa na kiu ya ‘kufa mtu’.
ATAKA KIDUME WA KUONDOKA NAYE
Vituko vya mrembo huyo havikuishia hapo kwani wakati ‘akigida’ kiroba,
alitaka ajitokeze kidume mmoja ili aambatane naye nyumbani kwake akamwoneshe kwamba yeye ni mwanamke wa shoka (bila kusema atakachokwenda kumfanyia).
ACHIMBA MKWARA, AINGIA UCHOCHORONI
Wakati ‘akifotolewa’ picha, alisikika akichimba mkwara kwamba endapo picha zake zitatumika gazetini au mahali popote, atamtoa mtu ‘mshipa’.
Alipofuatwa na Paparazi wetu kwa mahojiano, mwanamama huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Kwani wewe unanifahamu? Ole wako ukinitoa gazetini, Mungu wangu nitakufanyia kitu ambacho hutasahau hadi unakwenda ahera. Utanitafuta kuniomba msamaha ukiwa unatambaa.”
Alisema binti huyo akiingia uchochoroni na kupotelea kusikojulikana.

Mambo ya Pekechapekecha na Akudo
Bendi ya muziki wa dansi ya Akudo Impact, iKifanya onyesho lake katika Ukumbi wa Mango Garden.
Christian Bella akiimba huku mnenguaji wa bendi hiyo, Frida Joseph ‘Beckham’ akimnengulia.
Mnenguaji wa bendi hiyo Nane Esalaa akinengua huku sehemu kubwa ya makalio yake ikiwa nje..
Akina dada hawa nao hawakuwa nyuma katika kulicheza Pekechapekecha.
MKE AMLIPUA MUMEWE SEHEMU ZA SIRI
Mwanamke mmoja mwenye wivu wa mapenzi, Victoria Bynes (29) (pichani), amejikuta matatani baada ya kufikishwa mahakamani baada ya kuzichoma moto sehemu za siri za mumewe kwa kushuku kuwa ana kimada.
Habari za awali zinasema mwanamke huyo alichukizwa baada ya mume wake, Andrew Williams kulala nje ya ndoa kwa siku saba bila kurudi nyumbani na aliporudi alichukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye chupa na kummwagia sehemu za siri kabla ya kutumia kibiriti kuwasha moto ulioteketeza sehemu nyeti za mwanaume huyo.

“Wakati mwanaume huyo akihangaika kuuzima moto uliokuwa ukiteketeza sehemu zake nyeti, Victoria alipanda gari lake na kuondoka bila kumpa msaada wowote,” kilieleza chanzo cha habari.
Habari zinasema polisi walipoitwa walimkuta Williams akiwa ameungua vibaya sehemu za siri pamoja na tumbo lake, sasa yuko hoi amelazwa hospitali.
Ilielezwa kuwa sababu za mwanamke huyo kumchoma moto Williams ni kushuku kuwa ana kimada kwa vile hakurudi nyumbani wala kuwasiliana naye kwa muda wa wiki moja.
Tayari Victoria amefikishwa mahakamani kwa kosa hilo na alipoambiwa na hakimu ajitete alisema kuwa anajuta kwani aliziwasha moto nyeti za Williams kwa bahati mbaya, lengo lake lilikuwa kumtishia kuzichoma.
Subscribe to:
Posts (Atom)