Thursday, October 13, 2011

WATU 26 WAKAMATWA KWA MATUKIO YA UPIGAJI NONDO MKOANI MBEYA


Bwana Zefania Mwangwale mkazi wa Uyole ambaye ni miongoni mwa watu waliopigwa nondo akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.

WATU 26 wamekamatwa kwa kuhusika na matukio ya upigaji nondo mkoani Mbeya ambapo watuhumiwa wamegawanyika katika makundi matatu huku kila kundi likiwa na watu 4 hadi 15.

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi ameyataja makundi hayo kuwa kundi la kwanza linawahusisha watu wanne ambao ni Herodi Luka, Musa Idi, Fadhili Luvanda na David Jimy waliosababisha vifo vya watu wawili.

Kundi la pili lina watu saba ambao ni Edson Ulendo, Rashidi Mwakyungwe, Elasto Eliasi, Musa Isa, Amosi Mziho, Sifa Jolewa na Frenk Kitonga ambao walisababisha kifo cha Pc Meshaki

Kundi la mwisho linawahusisha watu 15 ambao wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi na kwamba kundi la kwanza na la pili yamekubali kuhusika na matukio ya upigaji nondo.

Wakati huo huo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, ametoa shukrani kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika kufanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa matukio ya upigaji nondo na kuwataka kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kudhibiti vitendo vya uhalifu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...