Sunday, October 9, 2011

KAZI NI KWAKO.... AUNT LULU UROJO....



MTANGAZAJI chakaramu Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amenaswa akiwa hoi kwa kilevi na kuwaacha wadau wakisema ‘kazi ni kwako’.


Kituko ni kwamba, Aunty Lulu alifakamia pombe hizo zilizompeleka hali ya ‘u-tilalila’ katika kipindi hiki ambacho anakabiliwa na mitihani ya kumaliza masomo ya uandishi wa habari ngazi ya stashahada.

Staa huyo aliyeanza ‘kuhiti’ tangu akiwa na umri mdogo, alinaswa na kamera zetu usiku wa Jumatano iliyopita ndani ya Club Bilicanas, Dar es Salaam.

Ilikuwa saa 6:39, paparazi alimtia machoni Aunty Lulu kwa mara ya kwanza ndani ya klabu hiyo, kulikokuwa na shoo ya Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.

Wakati huo, staa huyo alikuwa akirandaranda mfano wa mtu aliyekuwa akitafuta sehemu ya kujiegesha.
Baada ya kuzunguka kwa dakika mbili hivi, Aunty Lulu alitenga makalio jirani na moja ya kaunta za klabu hiyo na kuanza kukata monde a.k.a maji ya mende ambayo yalimchakaza na kumuacha hoi.

Kabla hajazimika, Aunty Lulu alifanya vitu viwili kwa zamu akiwa tayari rojorojo, kunywa pombe kwa fujo na kuchangamka kwa muziki wa Twanga, hivyo kukata mauno ‘kama hana akili nzuri’.

Kama ilivyo kwa msemo, ‘ulevi noma, funda moja tu la ziada linaweza kukuumbua’ ndivyo mambo yalivyomtokea puani Aunty Lulu, kwani mwisho alikuwa taabani na kufanya yasiyo na heshima.

Moja ya matukio ya kilevi aliyoyafanya ni kumvamia jamaa mmoja (anayedaiwa siyo riziki, pichani mbele) na kudendeka naye bila woga kabla ya kulala fofofo kwa kuugeuza ubao wa kaunta ndiyo kitanda cha chumbani kwake..

Baadhi ya watu wanaomfahamu Aunty Lulu waliamua kumuokoa kwa kumpakia kwenye teksi ili kumrudisha nyumbani kwao lakini muda huo, paparazi wa Risasi alishafanya kazi yake ya kuchukua picha.

KABLA HAJALEWA (JUMATANO JIONI)
 Jioni ya siku ya tukio, Aunty Lulu katika mawasiliano na mmoja wa mapaparazi wetu, aliandika SMS: “Jamani sasa hivi nipo ‘bize’ na masomo. Nipo kwenye mitihani ndiyo maana sipatikani.”

POMBE ZILIPOISHA (ALHAMISI ASUBUHI)
Baada ya kupigiwa simu na paparazi wetu kumjulia hali kutokana na jana yake kuwa tilalila alijibu: “Jamani mimi sikumbuki kitu, rafiki zangu ndiyo wameniambia asubuhi hii. Nadhani pombe sasa zinanishinda, hii ni hatari.”

CHUO CHA AUNTY LULU
Hivi sasa, Aunty Lulu anasomea cheti cha uandishi wa habari kwenye Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) jijini Dar.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...