Saturday, October 22, 2011

Comedy ZONE

Watu wakiwa wamejazana kwenyejazana daladala la kutoka mbagala kwenda kariakoo kwenye siti ya nyuma walikuwa wamekaa msela na sister du....

Msela akawa anatupia mistari kwa sister du kwa sauti ya kunong'oneza(kumtongoza), yule du akawa anamtolea nje.... Mbaya zaidi alikuwa anapayuka kwa sauti kubwa mpaka abiria wakaageuka kuwatazama...

Msela akamwambia tena sister du.... "Mbona mi naongea kwa sauti ndogo wewe unapayuka??!" Sister du ndio kwaaaaaaaanza akawa kachochewa.... "Bwana eee si useme unachotaka usinisumbue..." Tena kwa sauti kubwa zaidi ya mara ya kwanza..

Msela alipoona sasa abiria wamemtolea macho akaamua kumwaga mboga na yeye... "Wee msichana vipi??! Umejamba alafu nakueleza unajifanya mkali... Hutaki tukuambie kama umejamba....??! Dada sio ishu, nasema UMEJAMBA!!!"

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...