Saturday, October 1, 2011

Mastaa wajinadi KINGONO....

Imebainika kuwa baadhi ya mastaa wa kike Bongo waliojisajili kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook ili kutangaza kazi zao za sanaa duniani kote, wanatumia nafasi hiyo kujinadi kingono kwa wanaume.

The Udaku Master, limeifanyia kazi skendo hiyo kwa wiki kadhaa na kubaini ukweli asilimia 90.

Ilifahamika kwamba, baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakitumia njia hiyo mpya ya kisasa kujipatia ‘mabwana’ kwa kutundika picha zenye pozi za mahaba zilizoacha sehemu nyeti za miili yao ambapo wanaume huzipiga chabo na kuomba namna ya kukutana nao huku ahadi za kununuliwa magari, nyumba na fedha zikitumiwa kama chambo cha kuwanasa.

Baada ya kuziona picha hizo hasa zinapokuwa mpya ambazo hazijatumika magazetini, huziwekea maoni kwa kuzisifia kwa maneno matamu kama ‘your so sexy lady, hot, nice photos, glamour girl, angel’ na mengine ambapo staa husika hujibu ‘thanks my d’.

Katika mazingira hayo, baadhi ya mastaa hao huendelea kuchati na wanaume hadi kufikia hatua ya kutoa mawasiliano ya simu kwa ajili ya mambo mengine ya kimapenzi.

Ze UTAMU linashikilia mazungumzo ya mastaa lukuki wa Kibongo waliokuwa wakitokewa kimapenzi kupitia mtandao huo huku nao wakitoa ushirikiano mzuri wakijinadi kwa wanaume bila nongwa.

Wakizungumzia ishu hiyo, mastaa wenye picha za aina hiyo katika kurasa zao kwenye mtandao huo walikuwa na haya ya kusema:


REHEMA FABIAN
Mshiriki huyo wa Miss Kiswahili 2009, alifunguka: “Ni uamuzi wa mtu kuweka picha za nusu utupu au za ufukweni. Mimi sijinadi na kutongozwa ni haki ya mwanamke aliyekamilika. Uamuzi wa kukubali au kukataa ni wa mhusika.”


 RUTH SUKA ‘MAINDA’ 
Staa huyo alisema: “Wapo wanaofanya hivyo, lakini kwangu Facebook ni sehemu ya burudani hivyo sioni tatizo kuweka picha inayoonesha nusu wa mwili wangu kwani mimi mwenyewe mavazi yangu ni mafupi na hata ‘barafu wangu wa moyo’ analitambua hilo.”




 JENNIFER MWAIPAJA ‘SHUMILETA’ 
Muigizaji huyo alitambaa na mistari: “Huwa naweka picha nikiwa klabu na kuwafahamisha marafiki zangu niko wapi kwa muda huo na siyo kujinadi kwa wanaume ili wanitongoze.”



 JACQUELINE PATRICK
Modo huyo maarufu Bongo alifunguka: “Mara nyingi wanaoweka picha kwenye Facebook huwa wana biashara zao. Kwa mfano mimi najihusisha na mambo ya urembo ndiyo maana naweka picha ya aina yoyote ile kwa ajili ya kujitangaza kuhusu kazi yangu.”

 

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
Muigizaji huyo alisema: “Hilo silishangai kulisikia kutokana na baadhi ya Watanzania wengi kwanza hawajui maana ya Facebook. Ina maana Beyonce au Rihanna (mastaa wa mtoni) wenye picha kibao za utupu wanajiuza?”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...