Monday, October 17, 2011

Comedy ZONE

Kulikuwa na harusi ilifanyika kanisani, wakati misa ya ndoa ikiendelea, Mchungaji ikafika wakati wa kuuliza kama kuna mtu mwenye kipingamizi na ndoa...

Babu mmoja na mkongojo wake akaanza kujivuta taratibu mpaka mbele...

Bibi harusi alipomwona akapiga kelele "Mungu wangu..." akaanguka na kuzimia.... Bwana harusi naye akaanza kuangua kilio huku akisema, "Nilijua tu lazima siri zivumbuke na hii harusi lazima iwe na vipingamizi..."

Mchungaji akamgeukia yule babu na kumuuliza, "Ehee babu tuambie una kizuizi gani?"

Babu akajibu kwa kujivuuuuuta, "Kha, kule nyuma spika mbovu nilikuwa sisikii vizuri mjukuu wangu, nimeamua kuja mbele nisikilize na kushuhudia vyema harusi inavyoendelea..."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...