Thursday, October 13, 2011

Diva akwaa skendo kubwa ya usagaji...SISTADUU mwenye sauti tamu anayeendesha Kipindi cha Ala za Roho kupitia Radio Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ ameikwaa skendo ya usagaji baada juzikati kukiri kuwa anamtamani kimapenzi demu mwenzake na yuko tayari amuoe.

Kupitia ‘blog’ yake Diva alitundika kukiri kwake akieleza kuwa, ukweli asioweza kuuficha ni kwamba ana hisia za kimapenzi na mwanamuziki wa kike wa Marekani, Robn ‘Rihanna’ Fent na kama inawezekana yuko tayari amuoe.

“Nina hisia za kimapenzi na huyu binti Rihanna...sijawahi kumtamani mwanamke in my entire life, lakini jamani kiukweli namtamani Rihanna kimapenzi kabisa...sasa siwezi hata kujificha.

”Kuanzia mgongo na kila kitu..., if ndoa za jinsia moja zingekuwepo Tanzania na Rihanna ananiambia anioe...nakubali kabisa, yaani ananivutia kimapenzi, mtoto Rihanna ananichanganya sana,” aliandika Diva.

Baada ya kuipitia kwa makini habari hiyo iliyoonekana kuwashika wadau wengi mtandaoni, Ijumaa lilimwendea hewani Diva kupitia simu yake ya kiganjani na alipoulizwa kilichomfanya afikie hatua ya kufunguka maneno hayo alisema:
 “Mimi hata sijali, kama nimempenda kwa nini asinioe? Yaani ikitokea amekuja leo Bongo na akasema anataka kunioa nipo tayari tena bure kabisa, asitoe hata mahari.

“Unajua nini? Mila na tamaduni za Kitanzania na mimi ni vitu viwili tofauti, to me I don’t care (kwangu mimi sijali) hata kama watu watasema lakini kwa Rihanna Dah! Sijiwezi.”

Baadhi ya watu waliopitia habari hiyo walionesha kumshangaa staa huyo mwenye mvuto wa aina yake kwa kushobokea mambo ya usagaji ambayo ni kinyume na mila na desturi za Kitanzania.

“Dah! Huyu Diva mbona anakoelekea siko? Hafananii kabisa na hiki anachokisema, usagaji unapigwa vita sana hapa kwetu, sasa iweje yeye afagilie mapenzi ya jinsi moja?” alihoji Farida wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Blog hii ilinalaani vitendo vya kisagaji vinavyofanywa na baadhi ya wanawake hapa nchini na linamsihi Diva kujaribu kuzidhibiti hisia zake za kimapenzi kwa wanawake wenzake kwani anaweza kujikuta pabaya siku za usoni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...