Monday, October 31, 2011

MAHABA: Woga, aibu hupunguza kujiamini katika mapenzi


KARIBUNI mpendwa wa safu yetu inayopendwa na wengi na kuwashukuru wote wanaopoteza muda wao kunipongeza wengine kunikosoa ili kuiboresha.
Vilevile wapo walio na matatizo wanaoomba msaada ambao nashukuru umewasaidia wengi.
Kama ilivyo ada, umekaa mkao wa kula kutaka kujua leo nimekuja na mpya gani. Nasema hakuna jipya chini ya jua kwa sababu kitu mapenzi kilikuwapo tangu enzi ya mababu na hata hao waliyakuta tokea enzi ya Adamu na Eva.

Haya leo nina nini?
Nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wasomaji wangu waliolalamika juu ya matatizo wanayokumbana nayo katika kula chakula cha roho, wengi wanalalamika kuwa hawali chakula kilichokamilika.
Kwa mfano mtu anauliza; Mbona mpenzi wangu si mtaalam wa mambo flani?, wengine hudiriki kusema tangu waanze mapenzi na waume zao au wake zao hawajafurahia mapenzi na kushangaa kusikia mapenzi ya kukukolea hukufanya upandishe mashetani na kumaliza maneno yote mdomoni au kumfanya mwanaume atoe ahadi hata hasizo na uwezo nazo kwa kusema atakununulia ndege wakati hata baiskeli hana.

Yote hayo ni mtu kuguswa pale panapomfanya ajione yupo dunia nyingine na kujiona juu hayupo wala chini hayupo. Wao hujiuliza kulikoni wenzao wafaidi wao wasifaidi kwani wamekosa nini.
Swadakta swali zuri sana, kumekuwa na utamaduni wa watu wengi kuona aibu kuuliza jambo walisilolijua hasa katika mapenzi hii imepelekea watu kuwa wavivu kujifunza kwa kuona aibu kuuliza kitu wasichokijua kwa kuogopa kuitwa washamba.

Nani alikuambia wote wamezaliwa wanajua, usichokijua uliza usisubiri aibu ikukute kwa mpenzio, kuuliza nje au kutoa nje udhaifu wako.
Siku zote wasiojua huwa wajanja sana ili kuficha udhaifu wao lakini unauficha udhaifu wako wakati lazima uingie kwenye gemu.
Kwa kuwa aliyeuliza ni mwanamke, hata akielezwa bado utakuwa mzigo kwa kuwa hawezi kufanya vile kwanza ataogopa kukuelekeza mtindo flani au ufanye vipi ili kumridhisha kwa kujua ameupata nje na kulisaliti penzi lenu.-
Jifunze kwanza kabisa kumuandaa mpenzio hii kumfanya mpenzi ashikwe na ashki ya mapenzi na mwili kuwa tayari kwa tendo. Hakikisha mpaka sehemu zake zimelainika na kutoa ute unaokuruhusu kumuingilia bila maumivu wala kuweka michubuko.

Utajuaje mpenzi wako yupo tayari kama si muongeaji? Sikiliza sauti yake kama mihemo yake huwa kama mtu mwenye pumu hata mwili wake hulegea. Hapo ruksa kumuingilia.
Lakini wanaume wengi wamekuwa wajanja wajanja kwa kuficha udhaifu wao katika uelewa katika mapenzi matokeo yake kila siku kushindwa kumridhisha mpenzi wake kimapenzi.
Kama nilivyokwisha kusema mwanzo kama hujui bora uulize kwa mtaalam wa masuala ya mapenzi kupitia kona za mahaba ili kuliokoa penzi lako.
Huenda unaweza lakini hofu iliyokujaa moyoni hukufanya ushindwe kujiamini. Kuuliza si ujinga na kukaa mkimpya si ujanja. 

Comedy ZONE

UBABE NOUMAAAA
A man goes to a restaurant
and orders a chicken dish. By the
time the food isready and he is about
to eat, the waiter comes back
and says, "Sir, I'm afraid there has
been a mistake. You see, that police officer who is
sitting at the next
table is a regular customer of ours
and he usually
... orders the same dish. The problem
is, this is the last chicken in the house. I'm afraid I'll have to take
this
dish to him and arrange for
another dish for you!" The guy gets
really upset and refuses to give up
his food. The waiter walks over to the
other table and
explains the situation to the officer.
A few minutes later the officer
walks over to the man's table and
says, "Listen and listen good. That is MY
chicken you are
about to eat and I'll warn you,
whatever you do to that chicken I'll
do the same to you. You pull out one
of its legs; I'll pull out one of yours. You break one of its wings; I'll
break one of your arms!" The man
calmly looks at the chicken, then
sticks his middle finger in the bird's
rectum, pulls it out and licks it. He
then gets up, drops his pants, bends over and says, "Your
turn sir!!"

Sunday, October 30, 2011

Michael Jackson wa Tanzania


Comedy ZONE

Masela walikuwa wanavuta bangi Sehemu,kibiriti kikawaishia, wakam2ma msela akaombe Sehemu, msela akatembea mpk anarudi tena kwenye chumba kilekile, na akasahau kama ndo alipo toka, akawaomba kibiriti,
washikaji wakamwambia,"mwana we njoo ukae kuna msela 2mem2ma ametoka Sa hv atarudi" 
bila kujua ndo msela wao,
Bangi Noma....

Friday, October 28, 2011

MAHABA: Wanaojua kupenda ndiyo wanaolia kila siku




NI wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini Mungu amekujaalia afya njema na nguvu za kutosha kiasi cha kukufanya uendelee na mchakamchaka wa maisha kama kawaida.

Jamani, hii ni safu ya mashamsham, mahususi kwa masuala ya mapenzi kwa ujumla. Wapo wanaonitaka niingie ndani kuzungumzia mambo ya chumbani kama vile namna wanandoa/wapenzi wanavyoweza kudatishana wawapo faragha.

Ni sawa kwani hapa ndiyo mahali pake kuyazungumzia lakini niseme tu kwamba mengine tukakuwa tunaelekezana kwa njia ya simu kwani hayastahili kusomwa na kila mtu.

Wiki hii nataka kuzungumzia hili suala la machozi katika mapenzi. Mapenzi kiukweli yanawatesa wengi. Wapo ambao kila siku ni watu wa kububujikwa na machozi kutokana na yale wanayofanyiwa na wapenzi wao. Kuna wanaofikia hatua ya kujuta kwa nini wamependa, wanajuta kwa kuwa wanaona hawapati ile furaha waliyotarajia.

Hili linauma sana na niseme tu kwamba, tunapoingia kwenye uhusiano tuwe tayari kwa lolote. Kuna suala la kutendwa na kufanyiwa ndivyo sivyo na wale ambao mioyo yetu imetua kwao.

Mapenzi ni kitu cha ajabu. Leo unaweza kutokea kumpenda mtu kwa dhati kabisa na ukaamini huyo ndiye uliyepangiwa na Mungu awe wako wa maisha lakini matokeo yake unakutana na mazingira tofauti.

Unajikuta umeingia kwa mtu asiye na penzi la dhati kwako na mbaya zaidi mtu huyo hakuambii kuwa huna nafasi kwenye moyo wake. Atakukubalia kwa sababu tu aidha anataka akuonje au kuna kitu anakihitaji kutoka kwako (fedha au vitu vingine).

Hayo ndiyo mapenzi ya siku hizi, kumpata mtu anayekupenda kama unavyompenda ni bahati sana. Wengi tunapenda pasipo na penzi matokeo yake sasa ni majuto kila siku.

Kwa nini machozi?

Unajua mapenzi ni upofu, unaweza kuwa na mtu ambaye unaona dalili za wazi kabisa kwamba hakupendi lakini eti kuogopa kumkosa unasema huenda atabadilika. Bahati itakuwa kwako kama kweli atabadilika kwa kuwa wapo ambao kadiri siku zinavyokwenda ndivyo wanavyozidisha mapenzi.

Kwa bahati mbaya ukakutana na mtu ambaye haupo kabisa moyoni mwake, suala la kulia huwezi kulikwepa. Atakuwa anakutenda kila siku na kukufanyia vioja vya kila aina lakini kwa kuwa ndiyo umeshapenda, unajikuta unalia weee kisha baadaye unasahu na kuendelea naye eti ili usimkose, mh! Mapenzi bwana!

Ni sahihi kuvumilia?

Sisemi usimvumilie yule uliyetokea kumpenda lakini ninachoeleza ni kwamba, uvumilivu una kikomo. Kwa mfano umetokea kumpenda mtu lakini kila unavyojaribu kumuweka kwenye mizani unabaini umeingia sehemu isiyo sahihi, piga moyo konde kisha muache.

Usimpe nafasi mtu akayafanya maisha yako yakawa ni ya huzuni kila siku. Tambua una haki ya kupenda lakini huna haki ya kulizwa na mtu unayempenda. Kama anakuliza si ndiyo ujue kwamba hana mapenzi ya dhati na wewe? Sasa kwa nini umng’ang’anie?

Ni safari ya kumpata mtu sahihi

Wataalam wa mapenzi wanaeleza kuwa, wengi ambao wanaishi maisha ya kimapenzi yaliyotawaliwa na furaha walipitia hatua ya kulizwa.

Ni wachache ambao walibahatika kuwapata watu sahihi moja kwa moja. Hivyo basi kama huyo uliyenaye hakupi ile furaha uliyotarajia, elewa ni hatua ya kuelekea kwa mwingine ambaye huenda ndiye alipangiwa kuwa wako.

Muwahi kabla

Huyo anayekuliza itafika wakati atakuacha na naamini kwa kuwa utakuwa umempenda sana utaumia kupita maelezo. Kwa msingi huo, endapo utaona dalili za wazi kwamba hupendwi, unatakiwa kumuacha haraka kabla hajakuacha. Hiyo itakusaidia kisaikolojia kwani utakuwa umejiandaa kumkosa tofauti na ile unaamka asubuhi unakutana na sms akikuambia wewe na yeye basi, utaumia sana.

Comedy ZONE

Kuna Jambazi mmoja alienda kuvamia nyumba fulani hivi. Alipofika ndani alimkuta mke na mme wapo kitandani na hawana silaha yoyote ile, jambazi kuona vile alimshika mke na kumuwekea kisu shingoni, akasema "kawaida yangu kabla sijauwa mtu lazima nimfaham jina lake" MKE: Elizabeth....!!!!! .JAMBAZI: nimekusamehe maana una jina kama la Mama yangu.. Akamgeukia Mme.. kumwekea kisu tu: 
MME: William, lakini NYUMBANI, KAZINI NA MTAANI najulikana kama Elizabeth..

KIBOKO YA MCHINA: DAWA MPYA YA KUKUZA MAKALIO


BAADA ya zile dawa za Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti zilizotikisa Bongo na kubainika kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’ moja kuwa kubwa kuliko lingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili kufa ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka nyingine za kienyeji...

Uchunguzi uliofanywa kupitia kwa wataalam mbalimbali wa tiba za asili Bongo, ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa waganga wa kienyeji.

Ilifahamika pia kuwa hivi sasa dawa hizo zinachangamkiwa na wanawake ile mbaya wakiamini kwamba hazina madhara kama zile za Kichina.

NI MCHANGANYIKO WA MITI 60
Mmoja wa wataalam hao aliyezungumza kwa sharti la kutochorwa jina ili kutoharibu ‘biznesi’ yake hiyo alisema kuwa, dawa hiyo ni mjumuisho au mchanganyiko wa miti zaidi ya 60 inayopatikana kwenye misitu mikubwa hasa mikoani.

INAITWAJE?
“Nimeshakuambia ni mchanganyiko wa miti zaidi ya 60, haina jina isipokuwa mteja akifika anatakiwa aseme kama anataka ‘mzigo’ wa ‘saizi’ gani.”

UNACHAGUA KALIO UNALOTAKA
Mtaalam huyo alikwenda mbele zaidi na kuweka kweupe kuwa dawa hiyo ni kiboko ya Mchina kwani dozi na bei yake hutegemea aina ya kalio analolitaka mteja husika.

“Ukitaka dogo, la kati au kubwa, kila moja lina dozi na bei yake ‘so’ inategemea mteja amechagua la aina gani,” alisema mtaalam huyo.

 WATAALAM WA TIBA ASILIA WANASEMAJE?
Baada ya kukusanya data za kutosha, Ijumaa lilifanya mahojiano na wataalam mbalimbali wa tiba za asili ambapo walikuwa na haya ya kusema:

MJUKUU WA BABU
Mganga maarufu kwa jina la Mjukuu wa Babu anayepatikana Mwananyamala jijini Dar es Salaam alifunguka:
“Nakwambia hii dawa ni kiboko ya zile za Kichina. Ni dawa nzuri na kusema kweli watumiaji ni wengi. Ni mchanganyiko wa miti zaidi ya sitini ambao huwa unatoa aina moja ya dawa.

ZAWAVUTIA MASTAA
“Tatizo baadhi ya waganga wanashindwa kuwa nayo kwa sababu hawana uwezo mkubwa wa kuifahamu miti husika, mimi ninayo na nimeshawapa mastaa kibao wa Kibongo hasa wa Kinondoni, wametumia na wengi wao imewavutia.”

Listi ya mastaa wanaokwenda kwa mganga huyo na ambao wameonesha mabadiliko, Mjukuu wa Babu alisema: “Siyo utaratibu wetu kuvujisha habari za wateja wetu ‘so’ mtanisamehe kwa hilo.”

MASTAA WATOA USHUHUDA
Huku akiwa na mshtuko kusikia mastaa wanatumia, ‘vuvuzela’ wetu aliwainulia mkonga wa simu ambapo kila mmoja alitoa ushuhuda wake;

IRENE UWOYA:
“Sina uhakika na dawa yoyote ya kuongeza makalio kwani sijawahi kutumia na wala sina shoga aliyetumia ili kuthibitisha, kwanza ya nini? Kama huna, huna tu!”

BADRA:
“Sikubaliani na matumizi ya hizo dawa, kwanza ni kumkosoa aliyekuumba, utamsikia mtu anaapa kabisa kwa Mungu kuwa lazima awe kama mimi, Wema au Kajala na kweli baada ya muda unamuona amebadilika, mwisho afya yake inabadilika kwa kuwa ameilazimisha kuliko uwezo wake.” 


AGNES MASOGANGE:
“Kinachowaponza ni kuhadaika na umbo langu, hili umbo si la Kichina wala mganga wa kienyeji, ni kitu ‘orijino’ kutoka tumboni kwa mama, isitoshe kwa hapa Bongo sidhani kama utaalamu huo wa kuwa na dawa hizo za kukuza makalio upo, watu wasidanganyike na picha zinazochorwa kwenye mabango ya matangazo ya waganga, ni kuvutia wateja tu.”




KAJALA MASANJA:
“Siamini kama kuna dawa za kienyeji za kukuza makalio, ni uongo mtupu, ya nini kuhangaika? Kama Mungu amekunyima, amekunyima tu.”


JANETH ISINIKA:
“Nawaonea huruma sana wanawake wenzangu wanaohangaika na dawa za kukuza makalio, mimi naona kuwa mtu anayefanya hivyo basi ajue anaishi kwa kutegemea wanaume hivyo anatengeneza makalio awakamate kirahisi.”


SHILOLE: 
“Aku! Mimi sijawahi kutumia dawa ya kuongeza kalio, langu ni la urithi kutoka kwa bibi yangu. isitoshe kwa Mnyamwezi ni jambo la kawaida kuwa na wowowo.”
“Kama kuna watu wanatumia hizo dawa nawaonea huruma, nahisi hawayafahamu madhara yake kwani ni makubwa sana.”

SAUDA MWILIMA: 
“Mwanamke lazima ujiamini kutokana na ulivyoumbwa, siamini kabisa kama kuna dawa ya kienyeji inayoweza kubadilisha maumbile ya mtu.”



LULU: 
“Sina ‘komenti’ kwa hilo kwani sifahamu chochote, mimi ‘mgeni’ hapa Bongo.”


SINTAH: 
“Mimi najua hizo dawa zinapatikana China, kwa hapa Bongo sidhani kama zipo, kuhusu za kienyeji, ni kama yale yaliyotokea Loliondo.”




ZILISHAPIGWA MARUFUKU
Miezi kadhaa iliyopita, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilitangaza kupiga marufuku dawa za Kichina kutokana na kubainika kuwa na madhara makubwa kwenye maumbile ya mwanadamu.


Comedy ZONE

Wasifu wa marehemu

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi akainuka na kusema, "kinachofuata sasa ndugu wafiwa na marafiki wa marehemu ni kusoma historia fupi ya marehemu tuliyemzika hapa leo, karibu ndugu uliyeandaliwa kwa shughuli hiyo..."

Msomaji: "Ifuatayo in historia fupi ya marehemu tuliyemlaza ktk nyumba ya milele hapa leo...

>Marehemu alizaliwa juu ya mti ambapo mzazi wake alijihifadhi baada ya kukimbia mafuriko miaka 26 iliyopita.

>Hakubahatika kupata kazi ya maana alisoma mpaka darasa la 3 tu ambapo aliamua kuacha shule baada ya kuona elimu haina mpango kwake.

> Marehemu alikuwa kero kwa familia yake hasa kwa tabia yake chafu ya udokozi, uongo, uvutaji bangi, ubakaji wa mifugo na baadae ushoga.

> Mimi binafsi mjomba wake nimefurahishwa sana na kifo cha marehemu huyu kwani alishawahi kunipakazia kuwa nimekufa kwa kipindupindu kiasi kwamba ndugu wote wakakusanyika na kunililia msiba huku yeye akikusanya fedha za rambi rambi na kukimbia nazo!!

> Mtoto alitutia hasara sana kwani alikuwa mwizi wa vitu vya ndani,pesa,ndala na viatu mpaka vya wageni, nguo zozote zikianikwa nje na hata mboga jikoni. Hapa nilipo, mimi na mke wangu hatuna hata nguo za ndani kwani alishaniibia zote..

>Pia tumepoteza gharama kibao kumtafutia vyuo vya ufundu lakini aliishia kula ada na mwisho wa siku kuwa shoga tangu tarehe 06/04/91 hivyo ana expirience ya miaka 20 ya USHOGA.

> Marehemu hakuugua bali kifo chake ni cha kujitakia kwani kajiua kwa kunywa sumu ya panya baada ya kukosa nauli ya kwenda Mombasa kuhudhuria onyesho la taarabu na mduara.

> Kwa niaba ya familia, wazazi na ndugu wa marehemu tunatoa pongezi kwa Mungu kwa kutupunguzia kero na kwa wote wanaomdai marehemu mtatusamehe kwani hatuna uwezo wa kuwalipa kwa sababu tunajua ghalama yake itakuwa kubwa ila msihofu atawalipa mkikutana peponi.

>Ndugu wote wa marehemu tunamuomba sana Mungu asiilaze roho ya marehemu peponi na wala asimpumzishe kwa amani ila kama kuna mkong'oto huko ampe wa kutosha na kama ni moto awe kuni kabisa kwa shida alizotuletea duniani.. "

WOTE TUSEME AMEN!!!

WALIOKUFA KIBAHA WAZIKWA MAJIVU!!!


Mkuu wa chumba cha kuhifadhi maiti, Bw. Andrew Kaswalala,  akitoa miili ya marehemu katika friji muda mfupi kabla ya mazishi.
Mwili wa marehemu aliyeungua na kuharibika vibaya ukiwa chumba cha maiti.
Majivu ya marehemu kadhaa yakiwa ndani ya mfuko kabla ya mazishi!
WATU waliokufa katika basi la Deluxe lililopinduka na kuungua moto maeneo ya Kongowe, Mkoa wa Pwani, wakati likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, walizikwa jana katika makaburi ya Air Msae.
Mtandao wetu ulikuwepo kukuletea yote yaliyojiri hapo.

Kaswalala akiyaweka majivu hayo katika mifuko ya ‘Rambo’.
Mifuko ya majivu ya marehemu.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akilia wakati maiti zikiwasili eneo la makaburi.
Majeneza yakiwa yamepangwa kutolewa heshima na maombi na wananchi.
Mmoja wa wazazi waliopoteza watoto katika ajali hiyo akilia kwa uchungu wakati wa maombezi.
Hivi ndivyo marehemu walivyozikwa.
Picha ya mmoja wa marehemu walioungua vibaya katika ajali hiyo ambaye alikuwa akisoma chuo kikuu.
Mazishi yakiendelea.

Tuesday, October 25, 2011

PENZI LA SIRI NA MADHARA YAKE!!


Ni wiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima bukheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.
Mimi niko freshi kabisa na leo nataka kuzungumzia mada inayohusu penzi la siri na madhara yake. Kilichonisukuma kuandika juu ya mada hii ni kutokana mazungumzo niliyoyafanya na mmoja wa wasomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina la Alex mkazi wa Arusha akieleza namna alivyoingia katika aina hii ya penzi na kile kilichompata baadaye.

“Niliingia katika uhusiano na binti mmoja baada ya kutokea kumpenda sana ambaye tulikuwa tunafanya kazi sehemu moja. Katika maisha yetu ya kimapenzi akawa amenieleza kuwa, wazazi wake ni watu wa dini sana na hawataki kusikia kwamba ana uhusiano na mwanaume yeyote.

Akanieleza kwamba, pale kazini kuna watu wanawajua vizuri wazazi wake hivyo kama nampenda na nataka kuwa naye, nikubali penzi letu liwe la siri, yaani watu wasijue kama sisi ni wapenzi.
Maelezo yake hayakuniingia akilini kwani sikuwa na lengo la kumchezea bali ilikuwa tuanzishe uhusiano kisha baada ya muda nimuoe kabisa.

Kwakuwa sikuwa tayari kumkosa, nikaona nikubaliane naye kwanza huku nikiwa na lengo la kuja kumueleza baadaye kwamba, hakuna haja ya kuficha kwani sikuwa na nia mbaya.
Tukawa tunaendelea na uhusiano wetu kwa siri, siku moja nikashitushwa na tetesi kuwa, kuna mwanaume mmoja pale kazini kagombana na mwanaume mwenzake baada ya kubaini kuwa, wanashea penzi na demu mmoja ambaye ni yule aliyenikubalia tuwe wapenzi lakini kwa siri. Nilishangaa sana na sikuweza kuziamini tetesi hizo.

Nilijaribu kumuuliza lakini alikataa katakata huku akieleza kuwa, watu wanazusha tu. Kweli hakukuwa na mazingira yoyote yanayoonesha kuwa yule msichana alikuwa na mwanaume pale kazini lakini machale yakazinicheza.
Nikaanza kumuwekea mitego mbalimbali na siku moja nikagundua kuwa, kumbe yule binti hakuwa ametulia, ni kicheche ile mbaya. Amekuwa na katabia ka’ kuanzisha uhusiano na wanaume tofauti kwa siri. Nilichokifanya ni kuachana naye.”

Hayo ndiyo maelezo ya Alex ambaye alinisukuma kuandika mada hii ya leo yenye kichwa cha habari, penzi la siri na madhara yake.
Kabla sijaendelea, wewe msomaji wangu utakuwa umegundua kuwa, mtu yeyote anayekuambia penzi lenu liwe la siri ni lazima kuna kitu flani anataka kukificha.

Yawezekana ikawa kweli kuna sababu za msingi ambazo zinamsukuma kuwa katika penzi la sampuli hiyo lakini wengi ni matapeli tu.
Wapo watu wengi huko mtaani ambao wako katika penzi la siri na wengi ni wale waliooa au walioolewa. Unakuta mwanamke ameolewa lakini kutokana na tamaa zake anaanzisha uhusiano na mwanaume mwingine nje ya ndoa na kumuomba iwe siri kwani bado anampenda mumewe.

Na kweli wapo wanaofanikiwa kuishi kwa muda mrefu wakiwatumikia waume zao lakini pia wakiwatumikia wanaume nje ya ndoa kwa siri. Vivyo hivyo, waume za watu ni miongoni mwa wanaoanzisha uhusiano wa kimapenzi wa siri na aidha wake za watu au wasichana ambao hawakuolewa.
Ukiachilia mbali hao walio katika ndoa, cha ajabu sasa unakuta mtu hajaolewa/hajaoa anaingia katika uhusiano na mtu lakini anadai kuwa, penzi lao liwe la siri.

Hapo ndipo kwenye walakini. Hapo juu tumeona kwamba, wanandoa wanaingia katika uhusiano nje ya ndoa na kutaka iwe siri kulinda ndoa zao, je wewe ambaye uko ‘singo’ na unataka mtu wa kuwa naye maishani mwako, umepata lakini unataka penzi lenu liwe la kuibia, why? Kwanini?

Ninachokiona hapa ni kwamba, mtu anayeng’ang’ania kutaka penzi lenu liwe la siri atakuwa ni tapeli na inawezekana ama kaolewa, kaoa au ana mpenzi wake na tamaa zake ndizo zinamsukuma kuanzisha uhusiano na wewe. Huyu ni mtu ambaye unatakiwa kuachana naye mara moja kwani hawezi kuwa na ‘future’ na wewe.

Siku zote kwenye penzi la kweli hakuna usiri, usiri wa nini sasa? Wewe uko ‘singo’ na unataka uwe na mimi kisha unataka watu wasijue kuwa sisi ni wapenzi, kwanini nisihisi kuwa kuna kitu unataka kunificha?
Usikose kufuatilia sehemu ya pili ya makala haya ili uweze kuona madhara ya kuingia katika penzi la siri.

Mama Diamond amuokoa Wema asijiue...




WEMA Isaac Sepetu, Jumatano iliyopita ilikuwa siku ngumu mno kwake na kama si jitihada za mzazi, leo yangekuwa yanazungumzwa mengine.


Wema ambaye hana historia ya kumlilia mwanaume, amekamatika kwenye penzi la brazameni anayedatisha ‘maduu’, Naseeb Abdul ‘Diamond’, Jumatano iliyopita baada ya kuambiwa anaachwa, aliona bora ajisalimishe kaburini kwa kunywa sumu.

Busara za mama mzazi wa Diamond, Sanura Khassim ‘Sandra’ ziliokoa jahazi kwa kumlazimisha mwanaye arudiane na Wema ili mambo yasiharibike.

WEMA ALIVYODATA
Jumatano iliyopita mchana, Wema alipata taarifa kuwa Diamond ‘Platinumz’ alishazungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza uamuzi wake wa kumuacha jumla.

Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006-07, alipata taarifa hizo akiwa kwenye kambi ya kurekodi filamu kwenye Hoteli ya Lamada, Ilala, Dar es Salaam.

Tukio la kwanza, Wema alivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Diamond kwa hasira, akaanza kulia.
Baada ya kutafakari, Wema aliona mtetezi pekee ni mama mkwe wake, Sandra, hivyo alimpigia simu na kuangusha kilio cha “mama mkwe nisaidie mwanao asiniache.”

Utu uzima dawa, Sandra alimwita mrembo huyo nyumbani kwake, Sinza, Dar ili wazungumze. Mapenzi ya Diamond ndani ya Wema, yana nguvu kuliko kazi, kwa hiyo akaondoka kambini bila kurekodi na kumuacha prodyuza wa muvi hiyo, Suleiman Barafu akiwa na mshangao.

Barafu alikasirika lakini wasanii wenzake, walimshauri amvumilie Wema kwa sababu yupo kwenye mateso makubwa ya kimapenzi.
Wema alipofika nyumbani, alimvamia mama mkwe wake, ‘mchozi’ huo, akamlamba miguu, akasema: “Mama nampenda Diamond kuliko chochote, akiniacha sina pa’ kuweka sura yangu.”

Akamchanganya mama mkwe: “Sitanii mama, endapo Diamond ataniacha, sitakuwa na uwezo wa kubeba haya mapenzi makubwa niliyonayo. Nitakunywa sumu, nitakufa. Ila sitajali kwa sababu nitakufa kwa sababu ya penzi la mwanaume ninayempenda.”

Mama Diamond ‘Sandra’ kusikia hivyo, akapagawa: “Mkamwana afe juu ya nini?” Alimwita Diamond nyumbani wazungumze lakini muafaka haukupatikana.

KIKAO USIKU MZIMA TABATA
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda linajitosheleza kwa data kwamba Sandra alimlazimisha Diamond arudiane na Wema ili kuokoa uhai wa mrembo huyo.

Kwa Diamond, ilikuwa ngumu kukubali, akishusha madai kuwa Wema ni mvivu, hapiki chakula nyumbani, hafui nguo, kazi zote hizo zinafanywa na mama yake (Sandra). Ameshasikia mengi lakini siyo ishu, kubwa ni kwamba mrembo huyo anamlazimisha Platinumz amfukuze mama yake mzazi ili wawe huru.

Hata hivyo, mama mtu alipangua hoja za Diamond na kuwataka wamalize tofauti zao na kurudiana.
Kikao hakikuzaa matunda, saa sita usiku (Alhamisi), Diamond, mama yake, mjomba wake anayeitwa Saidi na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Hamisi, walizungumza kwa muda mrefu kuhusu hatima ya mastaa hao.

BUSARA ZA KIUTU UZIMA
Habari zinasema kuwa baada ya mvutano wa muda mrefu, Saidi na Hamisi walisimama upande wa Sandra, hivyo kushinikiza Diamond kurudiana na Wema.
Kutokana na shinikizo hilo, Diamond alinywea, akasalimu amri mbele ya wakubwa. 

WEMA KAFICHWA
Kumpata Wema kwa sasa ni kazi ngumu kuliko kumtafuta Mullah Omar, kwani simu yake imezimwa na vyanzo vyetu vimetutonya kuwa mrembo huyo amekatazwa na Diamond asizungumze chochote kwa rafiki zake wala kwa chombo chochote cha habari.

NENO LA DIAMOND
Gazeti hili lilizungumza na staa huyo Ijumaa akiwa Dodoma, alikokwenda kufanya shoo, hili ni jibu lake: “Ni kweli, mimi na Wema tumerudiana. Mama alishinikiza, kwa hiyo nikasalimu amri.”

KAULI YA FAMILIA
Mama wa Diamond hakupatikana lakini kaka yake, Hamisi alisema: “Dogo alikosea kumuacha mwenzake bila kumshirikisha mzazi wake.”

KWELI WEMA KANASA
Wema alishaachana na wanaume kadhaa ambao walibaki na sononeko, yeye hakujuta na alisonga mbele lakini kwa Diamond imekuwa tofauti.

Baadhi ya wanaume hao ni wasanii, Steven Charles Kanumba, Charles Gabriel Mbwana, Hartmann Osmund Mbilinyi na Jumbe Yusuf Jumbe.     

SAA 18 ZA MWISHO ZA MWISHO ZA GADDAFI


KUNA mvutano kuhusu mazishi ya marehemu Kanali Muammar Gaddafi, watu wa kabila la kiongozi huyo wa zamani wa Libya, wanadai mwili wa ndugu yao ili wauzike kwa heshima, wakati Baraza la Mpito linaweka ngumu na kusisitiza kwamba atazikwa kwa siri kubwa.

Ijumaa Wikienda, limenasa maisha ya Gaddafi saa 18 kabla ya kifo chake pamoja na danadana za mwili wa kiongozi huyo ambaye neno lake, harakati zake na fedha alizomwaga katika ufadhili, ndivyo viliwezesha kuundwa kwa Umoja wa Afrika.


Jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito (NTC), Mustafa Mohammed Abdul Jalil alitarajiwa kwenda jijini Misrata kutoa tamko kuhusu mazishi hayo.

Kwa mujibu wa mtu anayedaiwa alikuwa mlinzi wa Gaddafi kabla ya kumgeuka dakika za mwisho, saa 18 kabla kiongozi huyo wa zamani wa Libya kufariki dunia, alizitumia kusali na kuweka mikakati ya kuhama Jiji la Sirte.

Mlinzi huyo (jina limehifadhiwa) alisema kuwa katika saa hizo 18, Gaddafi alizungumza na wanajeshi wachache waliokuwa wamebaki wanamlinda na kuwaambia kwamba hategemei kurudi kutawala Libya na hadhani kama ana maisha marefu.
Hata hivyo, jina la mlinzi huyo limefichwa ili kukwepa hasira za watu wanaompenda Gaddafi kulipa kisasi. 

Aliongeza kusema: “Aliwaambia wapigaji kwamba wakipata nafasi warudi kuitetea Libya na wasikubali vibaraka wa Marekani na Uingereza wafilisi mali za Walibya.”

Alisema kuwa saa tatu kabla Gaddafi na timu yake, hawajaanza kutoroka, alizungumza na wanaye kwa muda mrefu lakini akawasisitiza: “Msiumie wala msifedheheke, wakati mwingine Shetani hutumia nguvu na kufunika haki dhidi ya batili.”

NENO LA MWISHO
Mlinzi huyo alisema, Gaddafi alijitetea kwa maneno mengi ili asiuawe lakini kauli maarufu aliitoa kwa njia ya kuuliza, “je, ninyi wanangu, mnaifahamu haki kwenye uongo?”

SAFARI YA KIFO
Alhamisi iliyopita (Oktoba 20, 2011), Gaddafi na timu yake, wakiwa kwenye magari ya kifahari, walikuwa wanahama kutoka Jiji la Sirte kuelekea mpakani. Inadaiwa walitaka kutorokea nje ya nchi, ingawa taarifa nyingine zinadai kiongozi huyo aligoma kuondoka na kusisitiza anangoja kufa kwenye ardhi aliyozaliwa.

Saa 2:30 asubuhi (saa za Libya), vikosi vya Nato na Ufaransa viliyashambulia kwa mabomu magari ya msafara wa Gaddafi. Magari 15 yaliharibiwa kwenye mashambulizi hayo, Gaddafi na timu yake walikwenda kujificha kwenye daraja la mtaro.

5:05 asubuhi, NTC ilitangaza kuwa ngome ya Gaddafi imekwisha na kilichobaki ni kutafuta masalia.
8:00 mchana, baada ya mapambano ya risasi kwisha, Gaddafi aligundulika yupo kwenye daraja la mtaro wa maji machafu amejificha.

8:45 mchana mwanaume mmoja mkazi wa Sirte aliliambia Shirika la Utangazaji la Reuters kuwa alimuona Gaddafi akipigwa risasi tumboni kwa bastola yenye ukumwa wa 9mm.

8:56 mchana, Reuters ilitangaza kuwa Gaddafi alifariki dunia kutokana na majeraha baada ya mapigano ya risasi.

9:00 mchana, wapiganaji wa NTC walianza kuzunguka mitaani wanashangilia kukamatwa na kuuawa kwa Gaddafi.
10:31 alasiri, AFP ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Muttasim amekutwa ameuawa jijini Sirte.

11:52 jioni, mwili wa Gaddafi ulifikishwa Misrata.

1:50 jioni, Aljazeera ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Saif al Islam naye ameuawa kwenye mashambulizi hayo. Ingawa taarifa za baadaye zinasema kuwa Saif mikono yake ilikatika katika mashambulizi.

WALIBYA WAPANGA FOLENI KUSHUHUDIA MWILI WA KANALI GADDAFI...



Mwanahabari wa Daily Mail, Andrew Malone, akishuhudia mwili wa Kanali Muammar Gaddafi.
Wakazi wa Libya wakishuhudia mwili wa Kanali Gaddafi na kuupiga picha.MAMIA ya wakazi wa Libya jana walikusanyika kushuhudia mwili wa Muammar Gaddafi mjini Misrata. Mwili wa Gaddafi ulikuwa umehifadhiwa katika chumba kimoja kilichopo eneo la biashara mjini Misrata, ambapo ulipelekwa siku ya Alhamisi alipouawa.

Wananchi hao wakiwa katika foleni kwenda kuuona mwili wa Kanali Gaddafi jana mjini Misrata.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...