Saturday, June 30, 2012

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNE 30



WEMMA: ‘Mama kanitia aibu’



Wema Isaac Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu hawapo vizuri tangu yale mahojiano aliyoyafanya mzazi wake huyo runingani wiki mbili zilizopita akiwachana marafiki wa staa huyo mkubwa wa picha za Kibongo...
ALIJISIKIAJE?
Akizungumza katika mahojiano maalum juzi Alhamisi, Wema alisema kuwa hawezi kusahau siku mama yake alipofanya ‘intavyu’ kwani aliposikia anaaza kutiririka ilibidi aipigie magoti runinga akiiomba inyamaze akidhani inamsikia.

TUJIUNGE NA WEMA AKITIRIRIKA!
“Kwanza sikuwepo wakati mama anafanya intavyu ‘so’ sikutarajia kama angezungumza vitu vya namna ile.
“Ni kweli mama yangu kama mzazi alikuwa na kila sababu ya kunizungumzia, alikuwa na uchungu na mwanaye sawa! Lakini ‘mai mom’ alipitiliza.”

ALITAKIWA KUHARIRIWA?
“Nadhani kuna vitu vilitakiwa kuondolewa kwa sababu mara baada ya kuzungumza, hali ilikuwa mbaya sana kuanzia kwenye mitandao ya kijamii na hata dada yangu alinipigia simu nikamweleza nilivyojisikia vibaya.”

KANITIA AIBU!
“Nilijua mama kanitia aibu lakini nikajikaza kwa sababu utakumbuka ndo’ kwanza nilikuwa kwenye maandalizi ya uzinduzi wa filamu yangu ya Super Star.
“Nilikaa kimya, nilijifanya kama hakuna kitu chochote kilichotokea lakini si unajua lazima moyo utakuuma tu hata kama ukijifanya kusahau.
“Baada ya kuona nipo kimya ‘aithinki’ siku iliyofuata alinitumia meseji mbaya na ninazo lakini hadi leo sikumjibu.”

TUNAWEZA KUSEMA ALIKUDHALILISHA?
“Yaah…ukweli ‘situwesheni’ haikuwa nzuri. Meneja wangu Martin (Kadinda) alimpigia mama na kumsisitiza mwaliko niliokuwa nimempa wa kuhudhuria kwenye uzinduzi wa filamu yangu lakini amini usiamini mama yangu hakuhudhuria. Kwa upande wa baba naye hakufika lakini alinipa sababu za msingi kabisa nikamwelewa na pia alikuwa akifuatilia kila kitu kwa kuchati na dada yangu kwani alijua niko bize.”

VIPI KUPELEKWA KWA WAGANGA?
“Sijui mama alipata wapi hiyo kitu ‘coz’ sijawahi na wala sijui mambo ya waganga kama alivyozungumza yeye.”

NISAMEHENI SANA
“Kwa yeyote aliyeguswa na mama kwa namna yoyote, naomba anisamehe sana. Yaani magazeti ya Global naombeni muwe wa kwanza kunisamehe kwani yule ni mzazi wangu pamoja na yote, nampenda sana.”

NENO LA RISASI JUMAMOSI
Wema ameamua kutoa la moyoni mwake akiamini kuwa yeye ni staa kwa hiyo ni kioo cha jamii, hataki kuwepo na chuki kati yake na vyombo vya habari, kwa maana hiyo AMESAMEHEWA.

Dk. Ulimboka apelekwa Afrika Kusini kutibiwa...


Gari la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo.

Mwenyekiti huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi ndani ya uwanja huo. 

Uchuro vifo vya mastaa


KATIKA hali ya kuendeleza uchuro unaofanywa na mastaa mbalimbali, msanii wa sinema za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ (pichani) hivi karibuni ametoa mwongozo wa mazishi yake yatakavyokuwa pindi akifariki dunia...

RANGI YA JENEZA
Jack amesema kuwa anapenda jeneza lake lipambwe kwa rangi ya fedha (silver) kwani anaipenda sana rangi hiyo.
“Japokuwa wakati huo sitakuwa nikijua kinachoendelea, naomba ndugu, jamaa na marafiki zangu wazingatie jambo hilo,” alisema.
NGUO ZA WAOMBOLEZAJI
Pia, staa huyo amepanga nguo vitakazovaliwa na waombolezaji watakaofika katika msiba wake ziwe za rangi ya pinki na nyeupe.
“Nawaomba ndugu na marafiki zangu wa karibu siku hiyo washone nguo zenye rangi nyeupe na pinki. Rangi nyeupe inawakilisha amani, japokuwa nitakuwa nimekufa, nitapenda kila mmoja abaki na amani kwani kila nafsi itaonja mauti.”
KWA NINI PINKI?
Jack amesema kuwa anaipenda rangi ya pinki na siku hiyo itakuwa inawakilisha upendo kwani yeye ni mtu wa upendo kwa kila mtu.
“Pamoja na kwamba sitakuwa najua kinachoendelea ulimwenguni lakini suala la upendo kwa kila mmoja ni la muhimu. Hivyo, nitapenda ndugu zangu waishi kwa upendo kwani hiyo ni amri kuu ya Mungu ambayo aliagiza tupendane.”

JIDE
Hata kabla ya mwaka haujakatika, msanii wa Bongo fleva, Judith Wambura ‘Jide’ naye aliweka wazi jinsi anavyotaka watu wavae siku ya mazishi yake.
Mbali na hivyo, Jide alitoa hadi mfano wa jeneza analotaka azikwe nalo.

JACK PATRICK NAYE
Naye mwanamitindo, Jacqueline Patrick hakubaki nyuma, alichukua fursa kueleza jinsi atakavyopenda azikwe baada ya kukata roho.

Bi Kidude achengua Dar...



Bi Kidude akiimba
Shabiki akimtunza Bi Kidude

Baadhi ya mashabiki wakiserebuka na milindimo ya Pwani

Jumanne Ulaya akicharaza gitaa

Mariam Hamis wa bendi ya TOT akiimba wimbo wa Paka Mapepe.

Mashabiki wakipozi juu ya jukwaa ili kupiga picha na Bi Kidude.

Mambo ya pwani hayo.

Saida Ramadhani wa Mshauzi akiimba huku shabiki akimkatikia.

Shabiki mwenye mzuka wa taarabu akiserebuka huku ameshikilia jukwaa.

Bi Kidude akionyesha umahili wake wa kucheza.

Mtangazaji wa Kituo cha TV Cha Sibuka Lulu akipozi kupiga picha.

Jana usiku katika ukumbi wa Equator uliopo Mtoni kwa Azizi Ally kulifanyika onyesho la taarab, wanamuziki mbalimbali wa taarabu waliudhuria akiwemo mwanamuziki mwalikwa toka Zanzibar Bi Kidude.
Baadhi ya bendi ambazo ziliudhuria onyesho hilo ni Five Star, TOT, East Africa Melod na Mashauzi Clasc
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...