Thursday, January 5, 2012

NDIKUMANA ABWAGA MANYANGA...




MASKINI! Ule uzi uliokuwa unashikilia ndoa ya Irene Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’ (pichani), umekatika rasmi baada ya mwanaume huyo kuamua kubwaga manyanga...

TUJIKUMBUSHE
Mara kadhaa, Ndikumana ambaye ni mwanasoka wa Rwanda amekuwa akiripotiwa kukumbana na mateso makubwa na kutofurahia maisha ya ndoa na Uwoya tangu Novemba, mwaka jana, mrembo huyo alipotangaza kuivunja ndoa yao ikashindikana.
NI ZAMU YA NDIKUMANA
Katika hali isiyotarajiwa, Ndikumana, bila kuuma maneno wala kupoteza muda, mwanzoni mwa wiki hii (Jumatatu) jijini Dar es Salaam, ilikuwa zamu yake kuvunja rasmi ndoa yake na Uwoya.
Tofauti na ilivyozoeleka kuwa Uwoya mara nyingi ndiye anayezungumza na vyombo vya habari, safari hii ni Ndikumana.

Ze UTAMU: Unasemaje Ndikumana? Au sijakuelewa?
Ndikumana: (Huku akiwa na jazba) Nimeachana rasmi na mke wangu Irene (Uwoya). Najiandaa kuondoka hapa nchini, lakini kabla ya kufanya hivyo, lazima nianike uozo wake wote. Ni muda mrefu sana nimemvumilia mke wangu, lakini sasa naamua kutoa yaliyomo moyoni mwangu, naamini ulimwengu ukiyasikia, utasikitika sana.
Ze UTAMU : Ha! Kisa nini lakini?
Ndikumana: Mengi yameandikwa juu ya ndoa yetu, lakini uozo alionifanyia Irene (Uwoya), nimeamua kuachana naye rasmi, sababu zipo nyingi, nitazieleza baadaye.

Ze UTAMU : Kwani hamkai pamoja?
Ndikumana: Kila mtu yuko kivyake.

Ze UTAMU: Je, ni kweli kwamba matatizo ya ndoa yenu yalianza Uwoya alipojifungua Krish (mtoto wao wa kiume) mwezi Mei, mwaka jana?
Ndikumana: Hata kabla ya hapo kulikuwa na matatizo.

Ze UTAMU: Sasa kama kulikuwa na matatizo mbona hamkuyasuluhisha yakaisha?
Ndikumana: Tulishakaa sana na wazazi, lakini mke wangu hakusikia.

Ze UTAMU: Ni hivi karibuni tu tuliwapatanisha baada ya ndoa yenu kuvunjika ‘then’ mkarudiana, huoni kama mtakuwa mnawayumbisha Watanzania?
Ndikumana: Ni kweli, nilidhani mke wangu amebadilika kama alivyoahidi mbele yenu, lakini ndiyo kwanza hali imekuwa mbaya, naomba niweke mambo sawa, keshokutwa Jumatano (leo) ndiyo nitapasua jipu rasmi kwa waandishi wa habari.

Ze UTAMU: Kwa kuwa umekataa kueleza sababu za kuvunjika kwa ndoa yenu kwa mara nyingine, basi dokeza kidogo hilo jipu utakalopasua litahusiana na nini hasa?
Ndikumana: Naomba nisivunje utaratibu wa siku hiyo, lakini ukweli ni kwamba nitataja hadi listi ya wanaume wake.

Ze UTAMU: Mh!
Ndikumana: Ndiyo, usishangae, najua uozo mwingi sana wa mke wangu, tusubiri, watu hawataamini, lakini ni kweli na nina ushahidi wa kutosha.

Ze UTAMU:  Je, baada ya kuachana na Uwoya, nini matarajio yako ya baadaye?
Ndikumana: Kila kitu nitakiweka wazi Jumatano (leo), lakini narudi Cyprus kucheza soka.

KRISH ITAKUWAJE?
Ze UTAMU: Vipi kuhusu mtoto wenu Krish itakuwaje?
Ndikumana: Nimekwambia mustakabali kamili ni Jumatano (leo) ndiyo nitakupa majibu kamili, nisingependa nijibu nusunusu.

MUDA WOWOTE NDIKUMANA ATAONDOKA
Habari za chini kwa chini zilieleza kuwa tayari Ndikumana amefanya taratibu zote za kuondoka Bongo mara tu baada ya kutoa siri ya mdudu aliyekuwa anatafuna ndoa yao.

UWOYA HAJULIKANI ANAKOISHI
Baada ya mazungumzo hayo, tulimtafuta Uwoya kwa udi na uvumba, lakini hakupatikana kwani nyumba wanayoishi, Sinza-Madukani, Dar, mlango ulikuwa umepigwa kufuli na nyumbani kwa mama yake, Mbezi Jogoo hakuwepo.

Uchunguzi wetu ulibaini kuwa wawili hao waliondoka Sinza-Madukani walipokuwa wamepangisha ambapo Ndikumana alirudi kwa mama mkwe (Mbezi Jogoo) kukaa na mtoto, lakini Uwoya haikujulikana anakoishi.

HISTORIA
Ndikumana alimuona Uwoya kwenye muvi ya Oprah ambapo ghafla moyo wake ‘ulimdondokea’ na kufanya taratibu za kumpata ndipo wakafunga ndoa ya kifahari iliyotafuna takribani Sh. milioni 80, Julai 11, 2009 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na kufuatiwa na sherehe ya kufa mtu kwenye Hoteli ya Giraffe View Mbezi Kawe, Dar.

Kwa mujibu wa Ndikumana, kwa sasa muvi hiyo kali imemalizika, lakini ili kupata kitu kamili na kusikia upande wa Uwoya...

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...