Tuesday, January 3, 2012

KINACHOMTESA NDIKUMANA KWA UWOYA...



Vitendo vya ufuska kwa wasanii wa filamu Bongo wanapokuwa maeneo ya kurekodi (Location), vinadaiwa kumpa mateso makubwa mume wa Irene Uwoya, Hamad Ndikumana ‘Kataut’...
Uchunguzi umebaini kuwa ni vigumu kwa baadhi ya wanaume kuvumilia wakiwaona wake zao wakifanyiwa vitendo vya kimahaba, hata kama wanaigiza.
Katika ripoti za gazeti hili, tumekuwa tukiainisha namna wasanii wengi wa filamu walivyo wachafu huku baadhi yao wakikiri kufanya kweli wanaporekodi vipande (scene) vya mahaba ambapo wao huhama kwenye kuigiza na kufanya ngono kiukweli.
KWA UPANDE WA NDIKUMANA
Lisemwalo lipo, kama halipo laja! Ili kujiridhisha na maneno hayo yaliyozagaa kitaani, hivi karibuni Ndikumana alitimba ‘lokesheni’ ambapo alishuhudia kwa macho yake mwenyewe bila miwani.
AMPIGA CHABO UWOYA  AKIFANYIWA MAHABA LIVE
Katika filamu iliyoingia sokoni hivi karibuni ya Dj Ben, kwenye matukio ya nyuma ya pazia (behind the scene), Ndikumana anaonekana akimpiga chabo Uwoya akirekodi kipande kinachomuonesha akifanyiwa vitendo vya kimahaba live.
AJIFICHA
Wakati Ndikumana ambaye ni mwanasoka wa Rwanda akifanya hivyo, mpiga picha (cameraman) aliigeuzia upande aliokuwa jamaa huyo ambapo hakuna jinsi zaidi ya kujitahidi kuficha sura yake.
ALISHAMKATAZA, HAKUSIKIA
Ndoa ya wawili hao ilipopigwa kimbunga ikitaka kufutika, Ndikumana aliliambia The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda kuwa alishamkataza Uwoya kucheza filamu za wasanii wenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Kanumba na Jacob Steven ‘JB’, lakini hakumsikia.
Alisema alijaribu kumwelewesha Uwoya kuwa afungue ampuni yake ya filamu kwani pamoja na yote, lakini hata fedha anazopata kupitia filamu za watu zinamtosha kwa ajili ya kununulia nguo tu kwa ajili ya filamu inayofuata.
Aliendelea kuweka kweupe kuwa alishamnunulia vifaa na kilichokuwa kimebaki ni kutafuta sehemu ya kuweka ofisi, lakini wakati hayo yakiendelea, mkewe alimgeuka na kurejea ulingoni kuigiza filamu za watu.
KAMA KUSOMA HUJUI, HATA KUANGALIA PICHA?
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wanandoa hao waliojaliwa mtoto mmoja wa kiume, Krish, Ndikumana aliposhuhudia vitendo hivyo, ndipo alipobadilika na kukosa raha muda wote.
Ilielezwa kuwa hata kama Ndikumana hakumwambia Uwoya alivyojisikia, lakini akimsoma atagundua kuna kitu kinautesa moyo wake.
AKONDEANA
Ni katika kipindi hiki ambacho Ndikumana amekonda hivyo kutoa mwanya watu kudai kuwa kinachomtesa ni kile alichokutana nacho lokesheni.
AOMBA APUMZIKE
Katika hilo, Ndikumana aliiambia blog hii: “Jamani please (tafadhali), niacheni nahitaji kupumzika na mambo hayo.”

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...