Tuesday, January 3, 2012

Harusi ya Mkwere FULL VITUKO...



Chereko, vifijo, shangwe, nderemo na vigelegele vilitawala kila kona ya ukumbi huku watu wakivunjika mbavu kwa vituko kwenye harusi ya komediani matata Bongo, Hemed Maliyaga ‘Mkwere’.
Tukio hilo lilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Delux Hotel Sinza, Dar es Salaam, usiku wa Ijumaa baada ya Mkwere wa Kundi la Mizengwe, kufunga ndoa na Fatma Abdallah Massawa siku hiyo mchana Mabibo, Dar.

MSOSI
Mnuso huo ulioshuhudiwa na ‘mashushu’ wetu ulianza saa 3:00 usiku kwa Mkwere kuwakumbuka wazazi wake waliotangulia mbele ya haki na baada ya hapo ‘mpunga’ ukaliwa kisawasawa.
Wakati mambo yakiendelea, Mkwere na mastaa wenzake wa Mizengwe wanaouza nyago kupitia ITV, Mzee Matata na Maringo Saba (best man) walikuwa wakiwavunja watu mbavu kwa maneno na vituko vyao.

SEBENE
Ulifika wakati wa sebene ambapo Mzee Matata, pamoja na umri wake kusogea, aliibuka nyota wa mchezo kwa namna alivyokata mayenu.

MZEE MATATA AVIMBIWA
Baadaye Mzee Matata aliwamaliza watu kwa kicheko alipotangaza kuvimbiwa na msosi hadi kushindwa kuinuka, hata hivyo ilikuwa ni sehemu ya vituko vyake tu kwani halikuwa tukio ‘siriaz’.

MKWERE AMEOA KIFAA
Kwa upande wake, Mkwere alitangaza kuwa aamini macho yake kama ameoa mwanamke mrembo kiasi hicho.

BIHARUSI AMTAMBULISHA MTOTO
Hata hivyo, biharusi alipokamata ‘maiki’ alisema mumewe alisahau kitu fulani kwani hakumtambulisha mtoto wao kipenzi, Camilla Hemed Mariyanga, ishu ambayo ilizua mjadala wa chinichini.
MASTAA

Baadhi ya mastaa waliohudhuria mbali na wale wa Mizengwe ni pamoja na Coletha Raymond na Lucy Komba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...