Friday, January 27, 2012

KIMENUKA... WEMA, KAJALA WAGOMBEA BWANA...



http://api.ning.com/files/v864S1k6upToZ0emQVN2OKNteDAr7*RTYRd59YJ-d0COBm8rzsqlCtO8-6wgFoDvuPyFIRql0RMhoufytkdPCNWTF7RvTXf2/kajalal.jpg
Kajala Masanja.
Wema.
KIMENUKA! Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja, wanadaiwa kuingia kwenye bifu ‘babkubwa’ kisa kikidaiwa ni kugombea mwanaume...

NI KIGOGO WA IKULU
Kwa mujibu wa chanzo kisicho na shaka, hivi karibuni warembo hao ‘wanaokinukisha’ katika tasnia ya filamu Bongo, walijikuta wakiingia kwenye gogoro kufuatia Kajala kutuhumiwa ‘kumtokea’ mwanaume mpya wa Wema aliyetajwa kwa jina moja la Clemence ambaye anadaiwa ni kigogo wa Ikulu.

Chanzo hicho kilidai kuwa Wema alimtambulisha Kajala kwa mwanaume huyo mwenye noti zake tofauti na msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ aliyekuwa ‘akiminya’ na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.

KAJALA ASAKA NAMBA YA GARI
Ilidaiwa kuwa, baada ya Kajala kutambulishwa kama shemeji, ulipita ukimya f’lani, nyuma kukiwa na madai kuwa alikuwa akisaka namba ya gari la jamaa huyo ili kumsaidia kufahamiana naye kabla ya kunasa namba yake ya simu.

“Asikwambie mtu, Kajala alipokosa namba ya simu, mwanzoni alikuwa akisaka mpaka namba ya gari, lakini Mungu si Athumani, alifanikiwa kupata ya kilongalonga ‘coz’ Wema aliachia mwanya fulani akijua ni shosti wake hivyo hawezi kufanya chochote.

“Kikulacho ki nguoni mwako, fumba fumbua Wema akapelekewa malalamiko na mwanaume kuwa Kajala anataka mambo,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki mkubwa wa wawili hao.

Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, baada ya Wema kufikishiwa ushahidi wa ‘sms’, kama kawaida yake, hakuhoji chochote zaidi ya kumvaa Kajala mzimamzima na kukinukisha na sasa hawaivi.

PICHA YA JOKATE, DIAMOND
Huku kikilionesha ushahidi kwenye mtandao wa BBM, chanzo hicho kilidai kuwa ishu hiyo ilihamia kwenye mtandao huo ambapo Kajala aliweka picha ya Jokate Mwegelo na Diamond akiandika: “Chezea Hao!”

Ilisemekana kuwa, picha hiyo ilitoa nafasi kwa wadau wa mtandao huo kumtukana Wema kwa kuweka maoni ya matusi. Habari zilizidi kuweka kweupe kuwa, Wema aliposikia ishu hiyo, alizama mtandaoni humo na kujionea mwenyewe.

WEMA AJIBU MAPIGO
Ilielezwa kuwa, katika vitu ambavyo Wema huwa hapendi ni kusikia au kutajiwa ishu ya Jokate na Diamond hivyo naye akajibu mapigo.

Ilifahamika kuwa, Wema naye alitafuta picha ya bwa’mdogo anayedaiwa kutoka naye aliyetajwa kwa jina moja la Petty Man akiwa kimahaba na kidemu kingine kilichotajwa kwa jina moja la Hamisa, hivyo Kajala naye akapokea za uso laivu kutoka kwa wadau wa mtandao huo.

Hata hivyo, pamoja na hayo, ilidaiwa kuwa Kajala hakufanikiwa kumnasa mwanaume huyo kufuatia Wema kuweka ulinzi mkali na kuvunja ushosti wao.

MSAKO KUWEKA HESHIMA MJINI
Chanzo kiliendelea kusema kuwa, baada ya wawili hao kutifuana kwa maneno, sasa wanasakana ili kushikishana adabu na kuwekeana heshima mjini.

KAJALA ANASEMAJE?
Kama kawa, kama dawa, baada ya mtiti huo kutua kwenye dawati, mtu wa kwaza kutafutwa ili kuweka wazi anachokijua ni Kajala ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Duh! Kweli nyie mnatisha, mimi sina ‘comment’ muulizeni huyo Wema.”

HEBU MSIKIE WEMA
Alipotafutwa Wema na kumwagiwa ‘upupu’ mwanzo hadi mwisho, alikuwa na haya ya kusema:
“Siwezi kugombea mwanaume na Kajala, ila kuna kitu kilitugombanisha.
“Huyo Hamisa ni mdogo wangu wa hiari ‘so’ nina uhuru wa kuweka kitu chochote kwenye ukurasa wangu wa BBM.”

Alipotakiwa kueleza hicho kilichosababisha wakagombana, Wema hakuwa tayari, lakini HOT POT inaendelea na mchakato kujua kisa na mkasa kwani ndiyo muvi imeanza, kaa tayari.  

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...