Saturday, January 28, 2012

Maskini vengu... Taarifa toka INDIA inasikitisha...

HALI ya msanii ‘jembe’ wa Orijino Komedi, Joseph Shamba ‘Vengu’ (pichani) imeelezwa bado ni tete huku kauli mbiu ikiendelea kuwa ileile ‘jamani tumuombeeni Vengu.’

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mtanzania mmoja anayefuatilia afya ya staa huyo nchini India alipo kwa matibabu, hali si nzuri licha ya kukutana na madaktari bingwa wa huko.

“Jamani cha kusisitiza ni kwa Watanzania huko nyumbani tuzidi kumwombea Vengu, bado hayuko vizuri, hali ni tete,” alisema Mtanzania huyo kwa kuweka mada kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook.


Baada ya taarifa hiyo ya kushtua, Jumanne wiki hii, mapaparazi wetu walitinga nyumbani kwa msanii huyo, Mabibo jijini Dar es Salaam ili kusikia chochote kutoka kwa familia yake.

Awali, mapaparazi wetu walizungumza na jirani mmoja aliyekataa kutaja jina lake ambapo alisema anachojua yeye, msanii huyo atarudishwa Tanzania ili familia ijaribu na dawa za mitishamba.

“Msiniulize sana mimi, kwao pale (akisonza kidole kuwaonesha mapaparazi wetu). Ila nasikia watamrudisha ili wajaribu dawa za mitishamba. Nasikia hali si nzuri,” alisema jirani huyo mwanamke.

Mapaparazi wakakanyaga hadi nje ya nyumba ya akina Vengu na kukutana na dada mmoja ambaye awali alisema pale sipo kwenye makazi ya msanii huyo, lakini alipobanwa sana alikiri.
“Haya, hapa ni kwa akina Vengu, mnasemaje?”

Utamu: Lengo letu kujua hali ya Vengu, anaendeleaje? Maana tumesikia hali ni mbaya kule India?
Dada: (bila kutaja jina lake) Vengu anaendelea… vizuri, lakini Watanzania wazidi kumuombea sana.
Licha ya jitihada za mapaparazi wetu kutaka kumdadisi zaidi, dada huyo alisema  yeye si mzungumzaji na kusema kama zinahitajika taarifa zaidi ya hapo basi kaka mkubwa wa familia ndiye anawajibika kwa hilo, lakini hakuwepo nyumbani muda huo.

KUNA SIRI INAENDELEA?
Siku hiyo mapaparazi wetu walipofika nyumbani kwao na staa huyo, mwanamke mmoja aliyeonekana ndiye mama mzazi wa Vengu alikuwa ndani amejiinamia wakati dada huyo akizungumza.
Mapaparazi walipomuuliza mwenyeji wao kama mwanamke huyo ni mama wa Vengu, alisema siye, ni mgeni alifika pale kusalimia tu.
Utamu: Tunamuomba nje tuongee naye basi.
Dada: Hakuna, haiwezekani.

KUMBUKUMBU NDEFU
Vengu, awali alilazwa kwa muda mrefu kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akikabiliwa na ugonjwa uitwayo kitaalam Brain au Cerebral Atrophy ambapo seli za kichwani hukosa mawasiliano na sehemu nyingine, pia mgonjwa hupoteza fahamu.
Hali ilipozidi kuwa tete, ‘komediani’ huyo alipelekwa Hospitali ya Apolo nchini India kwa matibabu zaidi.

Imesharipotiwa kwamba ili msanii huyo apone sawasawa matibabu yake yatagharimu shilingi milioni 320 za Tanzania.
KUTOKA KWA MHARIRI
Wapo Watanzania wengi wenye karama za maombi hata mgonjwa akiwa mbali, ni nafasi nzuri wakafanya hivyo kwa Vengu na wasanii wengine ambao hawana majina makubwa. Mungu awaponye wote. Amina.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...