Monday, January 23, 2012

Mtoto wa NDIKU utata....





PAMOJA na nguvu kubwa inayotumiwa na wahusika kutuliza tuhuma ya staa wa ‘picha’ za Kibongo, Irene Uwoya ambaye ni mke wa Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kuzaa na mwigizaji mwenzake, Kulwa Kikumba ‘Dude’, bado minong’ono mitaani inazidi kushika kasi mithili ya moto wa kifuu.


Uchunguzi umebaini kuwa baada ya skendo hiyo kuwekwa kweupe, watu walianza kufananisha picha kwa kulinganisha sura ya mtoto huyo aitwaye Krish na Dude wakipambanisha na Ndikumana.
“Kama kweli mtoto ni wa Hamad (Ndiku) na siyo Dude, kweli binadamu duniani ni wawiliwawili kwa namna mtoto huyo anavyofanana na Dude ukilinganisha na Hamad.



“Unajua picha inabeba meseji zaidi ya elfu moja hivyo kitendo cha watu kuanza kufananisha picha, ndicho kimeibua hayo yote. Hebu cheki mwenyewe, kweli ukianza kupambanisha picha, mtoto anafanana zaidi na Dude kuliko Ndiku, lakini kitaalamu siyo.



“Lakini kwa nini Dude? Mbona kuna watu wengi wako karibu na Irene na hawajahusishwa? Nadhani ili kumaliza utata, bora vipimo vya vinasaba (DNA) vichukuliwe ili tujue moja kuliko kila mtu kusema lake,” alisema mmoja wa mastaa wa filamu akiwa juu ya tuhuma hizo...



Ilielezwa kuwa tuhuma hiyo ndiyo chanzo cha kuyumba kwa ndoa ya Irene na mwanasoka huyo wa Kimataifa wa Rwanda.

MADAI YA SIKU NYINGI
Tangu mtoto huyo alipoanza kuonekana kwenye vyombo vya habari, siku chache baada ya kuona jua Mei, mwaka jana, kumekuwa na maneno ya tuhuma nzito kuwa siyo kopi ya jamaa huyo.

SIYO DUDE TU
Mbali na Dude kumekuwa na madai yakiwahusisha mastaa tofauti lakini zaidi ni kigogo mmoja serikalini ambaye pia ni mdau mkubwa wa burudani Bongo (jina tunalo).

UTETEZI WA DUDE
Mara kadhaa UTAMU ilimpa Dude nafasi ya kueleza kile anachokijua juu ya mtoto huyo ambapo alijitetea: “Hizi habari hata mimi nazishangaa, Irene ni msanii mwenzangu, ni rafiki yangu na hata mke wangu ni rafiki yake.



“Ukaribu wangu na Irene ulikuja wakati nafanya naye muvi, nahisi watu walituweka kwenye fungu la wapenzi kwa sababu hiyo ila ukweli ni kwamba siyo na sijawahi kuwa mpenzi wake.”
Baada ya kuona hali inazidi kuwa tete, hivi karibuni Dude alikuwa akimsaka Ndikumana ili kuzungumza naye juu ya suala hilo lakini alikana kueleza kiundani alichotaka kumwambia.
Hata hivyo, haikufahamika kama alifanikiwa kukutana naye.

UWOYA ANA SIRI MOYONI?
Mara zote Uwoya amekuwa akisisitiza kuwa mtoto ni wa Ndiku huku akibainisha kuwa siri ya baba wa mtoto huwa anakuwa nayo mama.



“Ni kweli anayejua baba wa mtoto ni mama. Ninachokijua mimi mtoto ni wa Hamad (Ndikumana).
“Hao wanaotajwa nafahamiana nao kama waigizaji wenzangu na marafiki tu, hakuna kitu kama hicho.
“Jamani! Ama kweli watu wana maneno, hivi huwa wanayatoa wapi? Kwa nini lakini? Hawajui hata sisi tunaumia? Hivi watu wanadhani mimi nina roho ya chuma? Hata mimi nina nyama kama wao, naomba waache kwani inaumiza kupita maelezo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...