Saturday, January 7, 2012

Comedy ZONE


Bibi kizee mmoja alikwenda Benki moja maarufu sana hapa nchini ili kuweka fedha zake. Alipofika mapokezi aliuliza, "Naomba kumuona meneja mkuu wa benki hii..."

Mfanyakazi wa mapokezi akamuuliza, "Unataka kumuona kwa shida gani?"
"Nataka kufungua akaunti"akajibu bibi..."

Akaunti inafunguliwa hapahapa mapokezi,sio lazima mpaka kwa meneja..." Akajibu mtu wa mapokezi...

"Mimi nataka kufungua akaunti ofisini kwa meneja maana nina pesa nyingi sana hapa..." akasisitiza yule bibi...

"Hata hapa unaweza kufungua kwa pesa hizo zote na zitakuwa kwenye usalama tu..."
"Kama hutaki kuniruhusu kufungulia kwa meneja basi nakwenda kufungua kwenye benki nyingine..." Akasema bibi huku akiwa amechukia...

Kuona hivyo mfanyakazi wa mapokezi akaamua kumpeleka kwa meneja. 
"Kwa nini mmeshindwa kumfungulia akaunti huko mapokezi??!" Akauliza meneja...
"Amesema lazima afungulie kwako na nilipomsisitiza afungulie mapokezi alitaka kuondoka..."

Basi meneja akaamua amfungulie yeye akaunti, Bibi akazitoa pesa, zilikuwa shilingi milioni kumi Taslimu hadi meneja akashangaa na kumuuliza, 
"Bibi inaonekana pesa hizi umezidunduliza kwa muda mrefu sana eeh?!"

"Hapana nimezipata juzijuzi tu..." 
"Umezipataje?" 

"Kwa kupinga na mtu."
"Kweli?!! Kupinga tu ndo hadi ukapata pesa zote hizo?!"

"Yaah,nimepinga tu, tena hata na wewe tunaweza kupinga tu..."
"Ehe,tunaweza kupinga vipi?" Akauliza meneja kwa udadisi...

"Kwa mfano,tunaweza kupinga kuwa kesho saa kama hizi, pumbu zako zitakuwa za square yaani pembe nne, kama zikiwa hivyo, wewe utanipa milioni kumi na kama zisipobadilika mimi ntakupa hizo zangu.."

Meneja kusikia hvyo akakubali mara moja na wakapinga, bibi kizee akaondoka...

Meneja alibaki akiwa na wasiwasi sana, hata alipotoka ofisini kila mara alikuwa anazishika pumbu zake kuona kama zimebadilika... Hadi siku iliyofuata asubuhi bado pumbu zake zilikuwa kama kawaida, saa nne asubuhi bibi kizee alifika benk kwa meneja akiwa ameongozana na jamaa mmoja nyuma yake...

"Eeh naona bibi umekuja.." Meneja akasema huku akiwa na wasiwasi ,mara moja akatoka kwenda chooni kwenda kuhakikisha kama pumbu zake ziko sawasawa, akakuta hazijabadilika, akarudi mara moja ofisini kwake...

"Haya bibi pumbu zangu hazijabadilika, si unaona ziko sawasawa?! Nimekushnda!!" Akasema meneja kwa kutamba...

Bibi kizee akamsogelea meneja na kumwambia kwa sauti ya chini chini, 
"Sawa baba lakini mi nitahakikishaje?!?
Njoo tu uzishike..." Alijibu meneja...
"Sawa lakini lazima uvue suruali nizishike pumbu zako nihakikishe vizuri..." Alisema bibi kizee..

Meneja akavua suruali na bibi akaanza kuzichezea pumbu za meneja...
Wakati akiendelea kuzichezea huku bila mabadiliko, yule mtu aliyeongozana na bibi kizee alikuwa anajibamiza ukutani kwa nyuma huku akijilaumu na kulia...

Meneja akashangaa na kumuuliza bibi...
"Mbna huyo jamaa uliyekuja naye anajibamiza ukutani? Huoni kama ataumia?"

"Heh he eeeh!! Huyo KALIWA..!!!" Alisema bibi na kuendelea...
"Nilipinga naye jana kuwa leo hii saa nne nitakuwa nazichezea pumbu za meneja wa benki kubwa hapa nchini, akakataa eti siwezi...Tulipinga shilingi MILIONI ISHIRINI NA TANO..!!! Hivi ishakula kwake....

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...