Monday, January 9, 2012

DJ FETY: Mimi ni jike dume...





Fatma Hassan ‘Dj Fety’.

MTANGAZAJI wa kituo cha redio cha Cloud FM, Fatma Hassan ‘Dj Fety’ amekerwa na kauli za watu wanaomfananisha na mwanaume huku akitoa kauli kuwa yuko pande zote.

Mwanadada huyo alizungumza hayo mbele ya paparazi wetu juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulikokuwa na Tamasha la Bongo 50 lililoandaliwa na Clouds Media Group pamoja na Kampuni ya Airtel.


“Leo nimevaa kike, sijui watasemaje maana nakerwa sana na watu wanaosema navaa kidume, mara mtindo wangu wa maisha ni kama mwanaume, mimi niko pande zote, yaani dume jike na watasema sana,” alisema Dj Fety huku akimuonesha mwandishi wetu viatu vya kike alivyokuwa amevaa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...