Sunday, January 22, 2012

Diamond ampa Wema vitisho



Wema Isaac Sepetu.
MWANAMUZIKI Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, (pichani juu), anadaiwa kumpa vitishio aliyekuwa mpenzi wake Wema Isaac Sepetu kufuatia kitendo cha mlimwende huyo kumbania penzi...

CHANZO
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Wema, vitisho hivyo vimekuwepo tangu wawili hao walipofarakana baada ya mrembo huyo kudai kumfumania Diamond na Miss Tanzania namba mbili 2006/07, Jokate Mwegelo.

“Sijui Wema alimpa nini Diamond, tangu kipindi kile unaambiwa amekuwa akimpigia simu na kumtumia ‘sms’ akimuomba warudiane ili waendeleze penzi lao kama mwanzo, lakini Wema hataki kumsikia.

“Mimi nimezungumza na Wema juu ya msimamo wake akaniapia kuwa ameshamwambia Diamond hawezi kumrudia tena, lakini jamaa haelewi,” alisema shosti huyo wa Wema na kuongeza:
“Baada ya kuona hapati kitu, Diamond amekuwa akimpigia simu na kumtumia meseji za vitisho akimchimba biti kwa kumwambia hata afanyeje yeye anaamini ndiye mumewe hivyo siku akigundua ana mwanaume mwingine, alimwapia kuwa atamfanyia kitu mbaya.”

Rafiki huyo wa Wema aliendelea kutambaa na mistari kuwa, baada ya Diamond kugonga mwamba kufaidi tena penzi la Wema, amekuwa akimuomba amwelekeze nyumba anayoishi Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam ili amuibukie, jambo ambalo Wema hakukubaliana nalo.

WAHUSIKA WANASEMAJE?
Kama ilivyo ada ya blog ya UTAMU namba moja kwa burudani Bongo, katikati ya wiki hii lilifanya jitihada za kusikia pande zote ambapo lilianzia kwa Wema akiwa kama mlalamikaji.

HUYU HAPA WEMA
Alipopatikana Wema na kumwagia mkanda mzima, alikuwa na haya ya kusema:
“Kwanza kabla ya yote, nataka kujua aliyewaletea habari zangu kwa sababu kwa sasa sihitaji kuzungumzia wala hata kulitaja jina la Diamond.

“Sioni faida ya kuzungumzia mambo yaliyopita, kwa sasa napanga maisha yangu mapya.
“Kwa jinsi nilivyosikiliza maelezo yako…(akitaja jina la mwandishi wetu), huyo aliyewaambia ishu hiyo kutakuwa na kitu anachokijua, lakini mimi naamini hakuna wapenzi wanaoachana na mmoja wao akashindwa kuomba msamaha kwa mwenzake.

“Ni kweli ishu hiyo ipo na inaendelea ila sitaki kuzungumza lolote kwa sasa kwani kuna hatua nazichukua ambazo ni siri yangu.”

DIAMOND VIPI?
Utamu ilipomtafuta Diamond ili kupata mzani wa habari hiyo, simu yake iliita bila kupokelewa.
Wema na Diamond walikuwa wapenzi mastaa waliong’ara kila walipokatiza ambapo mwanamuziki huyo alimvisha muigizaji huyo pete ya uchumba kabla ya kumwagana hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...