Friday, January 6, 2012

AJALI MBILI ZATOKEA ENEO LA MIKESE, MOROGORO



Basi la Taqwa lenye namba za usajili T 478 BBJ lililokuwa likitokea Burundi kuelekea Dar es Salaam baada ya kupata ajali.

Basi la Moro Best lenye namba za usajili T 846 BCU nalo likiwa limepinduka, pembeni ni abiria waliokuwa ndani ya basi hilo.

Lori lenye namba za usajili T 593 AGA linalodaiwa kusababisha ajali hizo baada kuegeshwa mlimani bila tahadhari.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Bi Adolphina Chialo akiongea na wanahabari eneo la tukio.

Juhudi za kuliinua basi la Moro Best zikifanyika.

...Basi hilo baada ya kuinuliwa.

Foleni iliyosababishwa na ajali hizo.
AJALI mbili zimetokea leo katika mlima wa Fulwe eneo la Mikese mkoani Morogoro zikihusisha mabasi mawili yaliyopata ajali kutokana na lori lililoegeshwa mlimani bila kuweka tahadhari. Ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa moja na nusu asubuhi ambayo imelihusisha basi la Taqwa lenye namba za usajili T 478 BBJ lililokuwa likitokea Burundi kuelekea Dar es Salaam, wakati ya pili ikilihusisha basi la Moro Best lenye namba za usajili T 846 BCU lililopinduka eneo hilo hilo baada ya kukuta lori lenye namba za usajili T 593 AGA limeegeshwa mlimani bila tahadhari.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Bi Adolphina Chialo amedai ajali zote mbili zimetokana na uzembe wa madereva ambapo wa lori aliegesha gari lake juu ya mlima bila kuweka alama yoyote wakati madereva wa mabasi walifika eneo hilo wakiwa katika mwendo kasi na kushindwa kuchukua tahadhari. Watu wapatao 43 wamejeruhiwa na hamna aliyefariki katika ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...