Friday, January 6, 2012

FREEMASONS WACHARUKA...



UTABIRI wa ujio wa zama za Shetani umeanza kutimia, alama kubwa inayofafanuliwa kwenye maandiko ya chapa 666 inazunguka duniani kote, hata Tanzania imeshaanza kutumika. Ufafanuzi unaotolewa na mitandao ya intaneti inayojihusisha na habari za imani zenye mrengo wa Shetani, unabainisha kuwa chapa 666 haipo katika mfumo wa namba ila ni alama iliyopo kwenye bidhaa mbalimbali.

Kutokana na ufafanuzi huo, imebainika kuwa chapa 666 ambayo ipo kwenye maazimio ya Freemasons kuitawala dunia, inapatikana kwenye bidhaa za viwandani kama maji, juisi, biskuti, unga wa sembe, ngano na nyinginezo. Uchunguzi wetu umebaini kuwa bidhaa zenye alama inayofafanuliwa kuwa ndiyo chapa 666, nyingi zinapatikana zaidi kwenye ma-supamaketi (maduka makubwa).

Blog hii imeng’amua kwamba magazeti yanayozalishwa na makampuni mawili Bongo (majina tunayahifadhi), hutolewa yakiwa na chapa 666 kwenye kurasa zake za mwisho. Upekenyuaji wetu umewezesha kubaini kuwa wafanyabiasha wakubwa maarufu watatu Bongo, bidhaa zao zote hutoka zikiwa na chapa 666.

Blog hiii imeelezwa kwamba wafanyabiashara hao, wanafanikiwa kwa kuinuliwa na mikono mirefu ya Freemasons kwa sababu nao ni memba wa jamii hiyo ya siri. Inazidi kubainishwa kwamba Freeemasons ni Dini ya Shetani kwa sababu wafuasi wake humuabudu Shetani, Lucifer ambaye pia huitwa Jini Mkuu.
Bidhaa nyingi kutoka nje zina alama ya chapa 666, huku nyingi zikifafanuliwa kutokana na mikunjo ya herufi za majina yao. Wataalam wamebainisha kuwa herufi za majina ya bidhaa husika, hukunjwa na kutengeneza muonekano unaokaribiana na umbile la Lucifer.

Bidhaa kutoka nje kuna mavazi hususan mashati na jeans kutoka Marekani, vinywaji vikali, baridi vilivyo na gesi, simu za mkononi na kadhalika. Uchunguzi wetu umegundua kuwa kampuni moja ya mtandao wa simu za mkononi Bongo, nembo yake hutengeneza chapa 666.

NI VITA YA IMANI
Maandiko yanasema kuwa nyakati za mwisho kutakuwa na tishio la dunia kutawaliwa na Dini ya Shetani ambapo zama hizo zikifika kutakuwa na mfumo utakaozuia mtu yeyote kupata huduma za kijamii mpaka awe mwanachama na atatambulika kwa chapa 666.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Freemasons wanatumia njia mbalimbali kuhakikisha ulimwengu mzima hakuna anayeamini uwepo wa Mungu na wanapambana kuhakikisha hata Yesu (Nabii Isa) atakaporejea akute hakuna aliye tayari kukombolewa.

Inaelezwa kuwa Freemasons ipo kwenye mkakati thabiti wa kuitawala dunia kabla ya Desemba 2012, hivyo imekuwa ikiratibu sera zake kwa kuangusha tawala za nchi mbalimbali ambazo viongozi wake wameshindwa kuendana na matakwa yake kama ilivyokuwa kwa Gaddafi.

MSIMAMO WA MAPADRI
Hivi karibuni, mmoja wa mapadri wa Kanisa Katoliki Mkoa wa Dodoma, alikataa gari la kutembelea ambalo lilisajiliwa kwa kuandikwa namba 666.

Padri huyo, alikataa kwa sababu namba sita zikiwa tatu, zinaashiria uwepo wa nguvu ya Shetani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...