SUPA staa wa Bongo, Wema Isaac Sepetu juzikati alionesha jeuri kubwa ya fedha pale alipomwaga minoti jukwaani akiwatuza wanamuziki wa Bendi ya Mapacha Watatu...
Tukio hilo lilitokea Januari 24, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Star Coco Beach, Dar ambapo bendi hiyo ilikuwa ikitumbuiza.
Awali, wakati nyota huyo anaingia kwa mbwembwe, mwimbaji wa bendi hiyo, Kalala Hamza ‘Junior’ alipeleka kinywa kwenye ‘maiki’ na kumtaja jina hali iliyowafanya mashabiki wageuke kumwangalia.
Hapo sasa, Wema alikwenda moja kwa moja jukwaani na kutoa minoti kisha kuimwaga chini kama majani yanavyopukutika kwenye mti baada ya kukauka.
Noti hizo ambazo paparazi wetu alizihesabu kwa harakaharaka wakati zikiokotwa, zilizunguka kwa wanamuziki wote wa bendi hiyo.
Baadaye mwanamuziki wa Bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ alipanda kuimba kama mwalikwa, na yeye alikutana na ‘mvua’ hiyo ya pesa hadi aliposhuka.
Hali hiyo iliendelea kila mara, mpaka baadhi ya mashabiki wakampachika staa huyo jina la pedeshee wa kike Bongo.
Hali hiyo iliendelea kila mara, mpaka baadhi ya mashabiki wakampachika staa huyo jina la pedeshee wa kike Bongo.
Wema alilikubali jina hilo na baadaye akaanza kujiita mwenyewe.
Mpaka anaondoka ukumbini hapo, Wema licha ya kwamba alikuwa ‘chicha’ kwa ulabu, pia aliendelea kujiita pedeshee wa kike huku akiwa ameshatumia shilingi laki tano za Kitanzania.
“Mimi ni pedeshee wa kike Bongo. Leo nimefikisha sadaka yangu kwa watu, maana hata Mungu anasema unapojua kupokea basi jua na kutoa kwa wenzako. Sasa hivi mimi pesa ninayo bwana, nina akaunti mbili, moja ya pesa ya Tanzania nyingine dola,” alisema Pedeshee Wema.