Sunday, October 21, 2012

VURUGU ZILIZOTOKEA KARIAKOO NA KULAZIMISHA FFU KUTUMIA NGUVU KUTAWANYA WATU. ...


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika Maeneo ya Kariakoo na viunga vyake kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika .

 
 Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. 

 Safari ya kuelekea Kituo Kikuu ilianza





Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) wakimwingiza katika gari muumini wa Kiislamu aliyekamatwa katika viunga vya maeneo ya Ikulu 

 Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo

Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki


 Mitaa ya Kariakoo na viunga vyake ikiwa imeimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mitaa ya Kariakoo leo

 Ulinzi uliimarishwa na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika mitaa ya Kariakoo leo

 Wanajeshi wakivinjari katika mitaa ya Kariakoo leo

 Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo

Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.
 
 
Watu hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.

Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.Picha  kwa hisani ya Happiness Mnal

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...