Sunday, October 21, 2012

P-square wakiperform Zimbabwe.....

Kundi la muziki kutoka nchini Nigeria la P-Square lilifunika vilivyo kwenye tamasha lao kubwa lililofanyika nchini Zimbabwe siku ya jumamosi ya Oktoba 13 jijini Harare. Tamasha hilo lililofanyika kwenye viwanja vya Clamis Arena jijini humo lilikuwa la aina yake baada ya kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu na pia wasanii hao walivyoweza kulishambulia jukwaa kwa staili tofauti za kudansi na kuimba.
Zaidi ya mashabiki 35,000 waliweza kuhudhuria tamasha
hilo la aina yake  huku wengi wakitaka kuwaona wasanii hao ambao ni gumzo kwasasa barani Afrika, Lakini kubwa zaidi ni mapaparazi kugombania kupata picha ya 'PETER OKOYE'aliyebadilisha muonekano wake wa nywele kama unavyouona pichani ili waweze kuuza kwenye vyombo vyao vya habari.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...